mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 8,860
- 11,554
Tabora ni maarufu kwa kulima tumbaku na uvunaji wa asali sio mazao ya chakulaTabora haipo..?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tabora ni maarufu kwa kulima tumbaku na uvunaji wa asali sio mazao ya chakulaTabora haipo..?
Uko sahihi,Dodoma ni kukame haiingii akilini kuizidi TangaTanga ,mahindi tunayo ya kutosha ,viazi ,machungwa ,,nyanya,Maharage halafu tupitwe na Dodoma 😀😀sio kweli bhana
Uko sahihi,mtoa mada anatuwekea sijui zabibu,kahawa hivi sio vyakula.Nafikiri ingefaa kila zao likawa na orodha yake ya mikoa kinara.
Mikoa inayozalisha mahindi,mpunga na maharage ndiyo hasa inalisha nchi maana ndiyo staple.
Zaidi ya mahindi Kuna kipi kingine Cha maana hapo Rukwa?Rukwa isiwepo halafu iwepo Kigoma!
Hauifahamu dodoma, inatosha kusema hivyoUko sahihi,Dodoma ni kukame haiingii akilini kuizidi Tanga
Dodoma kwenye Kilimo hapo ni uongo hata Hayo Mahindi unayaona hapo Kondoa mengi yanatoka Handeni Tanga labda karanga na ZabibuHauifahamu dodoma, inatosha kusema hivyo
Ata huko kibaigwa hupafahamu, kondoa chemba huko hali yake ya hewa huijui, bahi ya mpunga kwako ni msamiati, chamwino ya uwele, mtama, mahindi, ufuta, karanga nk kwako ni tafsiri ya jangwa. Mpwapwa ya karanga, mahindi, albeit nk si kitu kwako
kataviHabari za wakati huu wakuu,
Leo tunawaletea mada muhimu kuhusu "Mikoa 10 Inayoongoza kwa Uzalishaji wa Chakula Tanzania". Tanzania imebarikiwa na ardhi yenye rutuba na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo, na mikoa mbalimbali imejipambanua katika uzalishaji wa mazao ya chakula.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Usalama wa Chakula Tanzania Bara ya mwaka 2024, mikoa ifuatayo imeonekana kuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula:
1. Ruvuma: Inajulikana kwa uzalishaji mkubwa wa mahindi, ikichangia kiasi kikubwa katika akiba ya chakula nchini.
2. Iringa: Pamoja na uzalishaji wa mazao ya chakula, mkoa huu una utoshelevu wa chakula kwa asilimia 139.
3. Njombe: Mkoa huu umeorodheshwa miongoni mwa mikoa yenye uzalishaji wa kutosheleza wa mazao ya chakula nchini.
4. Mbeya: Inajulikana kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula, ikiwa ni pamoja na mahindi na mboga mboga.
5. Morogoro: Mkoa huu ni maarufu kwa uzalishaji wa mpunga na mazao mengine ya chakula.
6. Kagera: Inajulikana kwa uzalishaji wa ndizi, kahawa na mazao mengine ya chakula.
7. Kigoma: Mkoa huu unazalisha mazao kama vile mihogo, mahindi na maharage.
8. Mara: Inajulikana kwa uzalishaji wa mahindi, mpunga na mazao mengine ya chakula.
9. Dodoma: Pamoja na kuwa makao makuu ya nchi, mkoa huu unazalisha mazao kama vile zabibu, mtama na mahindi.
10. Manyara: Mkoa huu umejipambanua katika uzalishaji wa mazao ya chakula, hasa mahindi na maharage.
Ni muhimu kutambua kuwa, licha ya uzalishaji huu mkubwa wa chakula, baadhi ya mikoa bado inakabiliwa changamoto za lishe duni, hususan udumavu kwa watoto. Hii inaonyesha umuhimu wa si tu kuzalisha chakula kwa wingi, bali pia kuhakikisha lishe bora na matumizi sahihi ya chakula hicho.
Vyanzo vya Taarifa Hii:
1. Bunge la Tanzania: parliament.go.tz
2. Nukta Habari: nukta.co.tz
3. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS): nbs.go.tz
Kwa yeyote anayetaka uchambuzi zaidi wa takwimu hizi, tafadhali tembelea tovuti hizo kwa taarifa kamili.
Wadau,Karibuni tujadili na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuboresha zaidi sekta ya kilimo na kuhakikisha lishe bora kwa Watanzania wote.
Viazi kwa maana ya watu vilaza au😂Mkuu Njombe ni mzalishaji namba moja wa viazi Tanzania
Mbona hakuna mikoa ya pwani au samaki sio chakulaHabari za wakati huu wakuu,

Karanga,ufuta hivi sio vyakula.Hauifahamu dodoma, inatosha kusema hivyo
Ata huko kibaigwa hupafahamu, kondoa chemba huko hali yake ya hewa huijui, bahi ya mpunga kwako ni msamiati, chamwino ya uwele, mtama, mahindi, ufuta, karanga nk kwako ni tafsiri ya jangwa. Mpwapwa ya karanga, mahindi, albeit nk si kitu kwako
Umeishi kwenye wilaya zake zote -Makete, Ludewa, Wanging'ombe na Njombe?Njombe ni uongo, nimeishi Njombe labda miti na parachichi
Hii ni uongo eti Dar inaongoza kwa kilimo cha Nanasi na Maembe hayo mashamba yako wapi? Hapo wamechukua ya kwenye masoko yaliyotoka mikoani huko. Dar hailimi zao lolote labda kidogo minazi
Ni kweliHii ni uongo eti Dar inaongoza kwa kilimo cha Nanasi na Maembe hayo mashamba yako wapi? Hapo wamechukua ya kwenye masoko yaliyotoka mikoani huko. Dar hailimi zao lolote labda kidogo minazi
Mazao pwani Kuna mazao gani mkuuMbona hakuna mikoa ya pwani au samaki sio chakula