Mikoa 15 Iliyochangia Mapato Mengi kupitia Kapu La TRA Kwa mwaka 2015/26

Zanzibar wanaingiza pesa zaidi ya hizo ukitoa Dar
Siyo kweli.

Pesa za Zanzibar zinabaki.Zaniabr kutunisha matumbo ya wapiga kelele.wa Zenji


Kieneo kidogo, wabunge 55, Jimbo lina watu 2500.

Juzi wameanza tu kitafiti.mafuta, wakayatoa kwenye Muungano, waliposikia tuna gesi Mtwara, wanataka Mgawo.


Wanakopa, Bara ndio walipaji.

Peaa za Road Fund zimechotwa kwenda Zenji huku bara barabara mashimo tupu.
 
Najua inakuchanganya. Ipo hivi, safari hii Mbeya imekuwa nje ya Top 10, lakini kwa miaka mingi imekuwa ikiingia Top 10 or top 5.
Kimaendeleo haikuwahi kufanana na mchango wake kimapato. Wanajituma, wanapambana kuchangia pato la taifa, lakini vipaombele vya kimaendeleo vinapelekwa Kilimanjaro na Arusha, sanassna ambacho Mbeya ilikuja kuambulia ni mkoa kugawanywa na mapato kuathirika, lakini ikaendelea kubaki kwenye top 10.

Linapokuja swala la maendeleo, Mbeya inasahaurika kabisa, ndiyo maana ukiungalia mji ni kama haujapangika, umechakaa, yaani upo hovyo sababu unaendelezwa kwa jitihada binafsi za wananchi kila mmoja kwa wezo wake tofauti na mikoa mingine ambapo unakuta kuna standards sababu serikali na mashirika yanaenda kuwekeza kwa kujenga Mahotel, estates majengo ya ofisi n.k huku serikali nayo ikipeleka mafungu ya bajeti za kimaendeleo na kusimamia utekelezaji kwa wakati.
Ule Uwanja wa ndege wa Songwe kufikiwa tu maamuzi kuwa ujengwe ilikuwa ni vita, na hata fungu lilipotoka ili ujenzi uanze ikaibuka vita nyingine, wakina Lowasa wakipambana kuchepusha project ili fungu likaujenge Uwanja wa Arusha lakini akina Prof Mwandosya na Dkt. Mwakyembe na wenyewe wakasimama imara, bila hivyo, ule uwanja ingebaki story tu.

Angalia mradi wa barabara jinsi unavyosuasua hadi sasa wakati miradi ya barabara sehemu nyingine iliyokuja sawa au baada ya Mbeya inaendelea
 
Wana Mbeya wanajipigania
 
Kwanini hakuna hata mkoa mmoja kutoka Zanzibar?
 
Mkuu naomba unisaidie

Ukitoa mapato ya tra ni mapato Gani mengine nchi na mikoa hukusanya
1.Tozo za Madini,mirahaba,leseni nk
2.Magawio ya Mashirikanya Umma
3.Mapato ya ndani ya Halmashauri na Mikoa
4.Tozo mbalimbali za Wizara mfano faini za Polisi,leseni za maliasili,Latra,Wakala za serikali mfano parking fees,nk
5.Mapato ya mamlaka ya Bandari,viwanja vya ndege,bodi za mazao nk.

Kiufupi Mapato ni mengi sana na wakusanyaji ni wengi,yote yangeputia TRA ndio picha ya Mikoa ingeonekana vizuri
 
Tanga inashika nafasi ya 3 lakini ukienda maeneo mengi ya huo Mkoa miundombinu yake ni duni! Hela zote mnapeleka Zanzibar.
 
Tanga inashika nafasi ya 3 lakini ukienda maeneo mengi ya huo Mkoa miundombinu yake ni duni! Hela zote mnapeleka Zanzibar.
Jinga kweli,kwani imeanza awamu ya SSH kushika namba 3,miaka mingine pesa mlikuwa mnapeleka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…