Ok
Mkuu kwako Maendeleo ni kitu gani?
Maendeleo unayapima kwa kipimo gani?
Je maendeleo ni majengo?
Je maendeleo ni pesa?
Je maendeleo ni barabara?
Je unaongelea maendeleo ya mtu binafsi?
Je maendeleo huletwa na nani?
Je wewe umekaa unasubiri maendeleo yaonekane huko kwenu?
Labda nikusaidie maendeleo yanatafsiriwa kwa kutumia kanuni za uchumi ambazo pia zina mapungufu
Maendeleo hupimwa kwa pato la Taifa (GDP) ambalo sasa unaweza kujua kila mkoa au sekta imechangia kwa kiasi gani? Na pia unaweza kugawa pato la Taifa kwa idadi ya watu ukajua maendeleo yapo vipi?
Mfano maeneo yenye mali ghafi na viwanda n i rahisi kuona yamechangia pato kubwa kwa Taifa,Lakini tukiligawa kwa idadi ya watu wa eneo hilo yawezekana kuna umaskini wa kutisha
Mfano ,Mtwara kuna bandari na kuna kiwanda kikubwa cha cement ,Pia ndiko kuna korosho zinazoingiza pesa za kigeni ,Je mapato ya bandari ya mtwara na mapato ya korosho ni kiasi gani?
Baada ya sensa serikali ilitoa report ya maendeleo pia,Je hiyo miko ipo?lakini moja ya maeneo yenye hali mbaya ni Bukoba hiyo nina uhakika na niliona kwenye report ya takwimu
Mbeya jijo ina pato kubwa ,Je ukiona watu wa Mbeya wana maisha mazuri na wana maendeleo ?
Dar es Salaam pi ina pato kubwa ,Je ina maendeleo na watu wake wengi wanaoshindia mihogo unasemaje?