Mikoa inayoongoza kwa kutoa wasomi wengi Tanzania

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
1. Arusha - Ni mkoa wenye historia kubwa ya kutoa shule nyingi zinazoongoza kitaifa, watalii wengi wakifika Tanzania wamezoea kutoa misaada mingi Arusha ikiwemo ya kielimu, pia kuna shule nyingi International ambazo wanafunzi huenda kusoma vyuo vikubwa vya ulaya na Marekani.

2. Kilimanjaro - Wakoloni waliwekeza sana kwenye elimu, hata kabla ya uhuru wasomi wengi walitokea Kilimanjaro, Ni mkoa wenye shule nyingi zaidi Tanzania,

3. Kagera - sidhani kama kuna mkoa ambao watu wake wanapenda kusoma kwa asili kuzidi Kagera, elimu ni kama burudani, ila wapo nyuma kwenye miundombinu ya kielimu.

4. Mbeya - Ni mkoa uliojiwekeza vizuri kwenye elimu pia ni jiji la pili kwa kuwa na vyuo vingi nchi nzima.

5. Mwanza - ni jiji linalojitahiji kielimu ila miundombinu ya elimu inahitajika zaidi, mfano hadi leo Mwanza, licha ya kuwa jiji la pili kwa ukubwa na lenye watu wengi, hamna chuo kikuu chochote cha serikali.

Mara iliwahi kuwa mkoa unaotoa wasomi wengi kipindi nchi ikiwa chini ya mfumo wa kijamaa enzi hizo mkoa mzima watu 100 pekee wanaendelea sekondari, lakini kwa sasa ni wapo nyuma sana kielimu, Mara huwa inashika nafasi za mkiani kwenye mikoa inayofeli zaidi form 4, pia mwamko wa kusomesha watoto wa kike bado ni mdogo sana.
 
Mleta mada tuambie kwanza kwenu wapi ili tuone kama hujajipendelea, halafu pili kwanini umefanya research ya mikoa tano tu ukaitolea maamuzi!
kwanini usiweka orodha ya mikoa yote ili tujue wa mwanzo, wa kati na wa mwisho! bila kufanya hivyo ripoti yako itakua batili.
 
Mimi nipo Dodoma.

Hakuna haja ya kuweka mikoa yote kwasababu gepu ni kubwa sana ukiondoa hio michache,
 
Na hao ndiyo wanaopaswa kuongoza nchi siyo hawa wazaramo na wapemba ndo maana nchi inadidimia maana inaongozwa na vilalaza
 
Na hao ndiyo wanaopaswa kuongoza nchi siyo hawa wazaramo na wapemba ndo maana nchi inadidimia maana inaongozwa na vilalaza
Uongozi ni dhana pana na yenye vipengele vingi. Mafanikio ya kielimu pekee hayatoshi kuwa kipimo cha ubora wa kiongozi. Inawezekana kabisa mtu aliyepata Division III ya ukingoni akawa na sifa muhimu za uongozi kama vile weledi, mcha Mungu, uzalendo, uchapakazi, uwajibikaji, na kujali maslahi ya wananchi.


Vilevile, mtu mwenye Masters anaweza kukosa maadili ya uongozi na kujihusisha na vitendo kama matumizi mabaya ya madaraka, Ufisadi na Rushwa, ubaguzi wa kikabila, upendeleo (nepotism), kuonea wananchi, kutumia nafasi yake kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma, n.k.
 
Unaweza kuwa na valid and logical points lakini huyu mbumbumbu hapana, she is pushing the country into the abyss.
 
Unaweza kuwa na valid and logical points lakini huyu mbumbumbu hapana, she is pushing the country into the abyss.
Katika uongozi suala la elimu huwa linahitajika ila sio zito sana.

Kiongozi awe ameelimika au ana elimu ya kawaida sana kama hajali watu anaoongoza, hataki kuwajibika, ni mbaguzi, fisadi, n.k. huyo si kiongozi tena ni mtawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…