Mikoa ipi inalipa kuweka nyumba ya kupangisha?

Mikoa ipi inalipa kuweka nyumba ya kupangisha?

Wakuu mikoa inatofautiana kwa vipato vya wakazi wake. Sina shaka kuhusu Dar linapokuja suala la mzunguko wa hela.

Tupeane abc za mikoa yenye vipato vilivyosimama (ukiondoa Dar) na kuna hela nzuri ya pango kwa hizi nyumba za kawaida za kupangisha (ambazo sio lodge).
Zanzibar
 
Dodoma vyumba ni bei ghali kuliko mikoa yote Tanzania, wanaoishi watakuja kukazia, Chumba cha Elfu 80 Dar Dodoma ni 120.
 
Mkoa gani hauna wapangaji? Wafanyakazi wa serikali, sekta binafsi n.k katika huo mkoa wote wamejenga majumba yao, sivyo?
Sawa kila mkoa una uhitaji ila hapo watu wanatazama faida ( kwa namna wamewekeza) Kuna baadhi ya mikoa nyumba ya kisasa kabisa ya vyumba vitatu ila unakuta kodi sh laki moja na nusu/ mbili... Kwa Dsm ni nadra kupata nyumba kwa bei hiyo..
 
iyo laki mbna nyingi sana kuna jamaangu alipanga mkoa flani akilipa 50k nyumba nzima tena ile self contained. sa huo si ufala wakati lile sinki moja tu la choo si chini laki unusu
 
Nenda Dodoma,ila Kwa tahadhari maana Watumishi wanaochangia demand pole pole Wanajenga Nyumba zao.Wakati Niko Dom baada ya serikali Kuhamia tulilipishwa hela kubwa za Kodi,ila pole pole zimeanza kushuka.Fikiria pia Geita Mjini,hasa Mitaa iliyopangika ya Barabara ya Kasamwa Hadi zipo Ofisi za Mkuu wa Mkoa.Bei za Viwanja hazijatisha bado na Huduma za Kijamii zipo vizuri.Geita Pana Kampuni ya GGM ina wafanyakazi Kari ya 3000,na pia Pana Watumishi wa Umma wa Ofisi 3 (RAS Geita,Geita TC na Geita DC).Pia Pana wafanyabiashara wa Madini na Vitu vingine.Population pia inakuwa Kwa a kasi.Hautajuta,Kodi za 5m to 6m Kwa Mwaka ni kawaida Kwa Nyumba ya 2 to 3 bedrooms.
 
Wakuu mikoa inatofautiana kwa vipato vya wakazi wake. Sina shaka kuhusu Dar linapokuja suala la mzunguko wa hela.

Tupeane abc za mikoa yenye vipato vilivyosimama (ukiondoa Dar) na kuna hela nzuri ya pango kwa hizi nyumba za kawaida za kupangisha (ambazo sio lodge).
Mikoa ya Tanzania inatofautiana kwa vipato vya wakazi wake. Ukiondoa Dar es Salaam, mikoa mingine yenye vipato vya juu kwa wakazi wake ni pamoja na:
  1. Iringa: Pato la wastani la mtu mmoja ni takriban Shilingi milioni 4.49.
  2. Kilimanjaro: Pato la wastani la mtu mmoja ni takriban Shilingi milioni 4.07.
  3. Mbeya: Pato la wastani la mtu mmoja ni takriban Shilingi milioni 3.79.
  4. Ruvuma: Pato la wastani la mtu mmoja ni takriban Shilingi milioni 3.69.
  5. Arusha: Pato la wastani la mtu mmoja ni takriban Shilingi milioni 3.65.
Uwekezaji wa nyumba za kupangisha katika mikoa yenye vipato vya juu ndiyo unaweza kuwa na faida kutokana na uwezo wa wakazi kulipa kodi za juu na mahitaji ya makazi bora.

Pia, viwango vinaweza kutofautiana kulingana na eneo, ukubwa wa nyumba, na huduma zinazotolewa katika hiyo nyumba.

Ova
 
Maeneo yenye machimbo ya madini (hususani dhahabu) kuna uhitaji mkubwa WA Nyumba/Vyumba Vya kupanga.

Na-suggest: Arusha, Geita, na Chunya -mbeya
 
Back
Top Bottom