Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kigoma inarudisha nyuma uchumi wa nchi kwa watu wake kuzaa bila mpangilio

Unajua elon musk ana watoto wangapi? Anao 12 na kachoka kutumia paipu sshv anafanya tu invitro fertilization

Ni nature yetu waafrika kuzaa sana, lkn sion ubaya wowote. Kukiwa na watoto wengi kunakua na probability kubwa ya kupata vipaji vingi, japo ni double edged sword
 
Mi pia natamani watoto wengi tatizo hao watoto una uwezo wa kuwaoatia mahitaji?au unawazaa wateseke
 
Wachaga wako wachache!? Wachaga wanazaliana ni wengi sana kama serikali ingekuwa inafanya sensa mwezi wa 12 wangefika hata million 3 na kuendelea ...Wachaga wanaishi mikoani wakizaliwa kule basi wanasepa kweny kutafuta maisha ..

Kuna asilimia kadhaa ya wachaga wamezaliwa mkoani , kule moshi wanaenda tu .

Tanzania yote ni wamoja kokote kule watu wanaenda , kwa hiyo usipime kwa kuangalia watu wanaokaa kilimanjaro tu .
 
Ukuaji wa wingi wa watu , hao wa kigoma na kanda ya ndio wanakimbilia Dar....Hao watu wa kigoma na kanda ya ziwa kila mkoa wapo
Wanatafuta fursa ya biashara 😂😂

Wanazaana harafu wanakimbilia Mikoa ya wenzao 🤣🤣

Mwisho,hata hivyo unawaonea ,Ukuaji wa watu Dar uko chini ya Wastani wa kitaifa,walaumu Wasukuma
 
'kila mtoto anakuja na sahani yake'

'mtoto ni baraka'

'tajiri na pesa zake, maskini na watoto wake'

imani za watu hizi mkuu, imani ni ngumu kuondoa
Katikankitabu chake "Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere And The Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960 -1964", rafiki yangu Profesa Paul Bjerk aliandika kuwa, serikali ya kwanza ya Tanganyika, mara baada ya uhuru, ilikuwa na ari kubwa sana ya maendeleo.

Ikaweka mipango mingi ya maendeleo.

Baada ya miaka mitano, kwenye kuangalia utekelezaji wa mipango ile, serikali ikakuta kuwa licha ya kukamilisha mipango mingi, bado mipango ilikuwa haijakidhi mahitaji, kwa sababu, mipango haikuzingatia sana ukuaji wa idadi ya watu.

Tatizo (kama utaliona tatizo) la ukuaji wa idadi ya watu jwa kasi, lilijulikana tangu mpango wa kwanza wa maendeleo ulipoisha, mwaka 1965.

Lakini, cha kushangaza, mpaka juzi hapa, rais Samia ameliongelea tatizo hilihili. Tena kaongelea tatizo kama ni jipya. Wakati linajulikana kwa miaka takribani 60 iliyopita.

Moja ya sababu tatizo linaendelea hivi, ni serikali kutolichukulia kwa umuhimu yake. Mfano mzuri, serikali ya tais Magufuli ilipuuzia suala hiki, na hata rais kuwaambia watu wazae tu, yeye atasomesha.

Wengi wakihusisha kauli hiyo na imani yake ya Kikatoliki inayotetea watu kuzaana sana, kwamba rais aliacha kutekeleza sera rasmi za nchi, na kuchomeka imani zake za Kikatoliki katika kuongeza nchi.

 
Huu uzi bila takwimu ni chai.
 
Elimu na Uchumi vikiongezeka matokeo yake ni kupungua Kwa uzazi.

Kule kwenye uzazi mkubwa Kuna ujinga na umaskini zaidi.
 
Wanatafuta fursa ya biashara 😂😂

Wanazaana harafu wanakimbilia Mikoa ya wenzao 🤣🤣

Mwisho,hata hivyo unawaonea ,Ukuaji wa watu Dar uko chini ya Wastani wa kitaifa,walaumu Wasukuma
Waha wanajaa kwenye treni wakati wa kuja Dar ila kurudi treni ni jeupe...Hao jamaa hawarudi kwao ni wauza vyomba maarufu hapo kariakoo.

Waha ni wakazi rasmi wa Dar wanatambulika kwa biashara zao .
 
Kwamba watoto wakishazaliwa tu wanasepea kwingine kwenda kutafuta maisha?
 
Binafsi ni mtu naeunga mkono watu wazaane japo sipendi kuishi Miji yenye Msongamano mkubwa wa watu.
 
Idadi ya watu kuwa kubwa huchangia uchumi kukua maana serikali hupata Kodi nyingi.Tatizo ni hatuna viongozi wazalendo.idadi ya watu wa china ni sawa na idadi ya watu bara zima la afrika lakini china imepiga hatua kubwa Kwa sababu ya uzalendo wao Kwa Nchi yao
 
Mkoa unawezaje kuwa na growth rate ndogo hivyo na birth rate kubwa kama unavyodai?

Birth rate si ndiyo inaleta growth rate, minus emigration and death rate?

So how do you explain a region with such a low growth rate and a high birth rate?

That is a contradiction.
 
Kigoma unayoitaja haipo kwenye Mikoa ambayo watu wanazaana sana tena Iko chini ya Wastani wa kitaifa,labda una chuki binafsi 👇👇View attachment 3065256
Hapa kuna scerio 2,
Nadhani alituma growth rate na sio birth rate. Population ya sehemu inaweza kukua kwa kuzaliana sana na immigration. Kigoma inaweza kuwa na birth rate kubwa lakini watu wakawa wanakimbilia mikoa mingine.
Zu Geita watu wanazaliana halafu hawahami maeneo yao. Etc
 
Alichoandika ni chuki na si utaalam. Mbona Wa visiwani eneo lao dogo na lina idadi kubwa ya watu. Kama huna uzazi tulia utalea watoto wa wenzio
 
Nimelifikiria hilo ndiyo maana nikaweka growth rate kama matokeo ya birth rate, net emigration na net death.

Lakini, nikafikiri kwamba, ili Kigoma iwe karibu ya mwisho hivyo kwenye growth rate, inabidi kuwe na net emigration kubwa sana ambayo tungeisikia tu.

Yani hata baada ya kufikiria emigration, Kigoma's growth rate is too low.

So what gives?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…