Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kigoma inarudisha nyuma uchumi wa nchi kwa watu wake kuzaa bila mpangilio

Napinga hoja yako mkuu.
nchi yetu bado sana tuna maeneo mengi sana ya wazi ambayo hayajagushwa toka dunia iundwe.
Hayo maeneo ya wazi sio ya kwako(huwa kuna raia wengi wajinga wajinga wakikuta eneo liko wazi wanajikalia tu halafu wakija kufurumishwa na mwenyewe tunaona wanavyopiga mayowe kumlilia Rais), pia hayo maeneo ya wazi sio ya binadamu pekee, Nchi yako inategemea utalii kama chanzo kikubwa cha mapato kwa hiyo maeneo mengine ni kwa ajili y Simba, Sokwe, fisi, tembo, nyati n.k. Mkiyamaliza maeneo ya utalii mtapiga miyao zaidi kwa njaa na ukata.
 
leo hii nani hawajui wanaijeria,dunia nzima wame jaa kutokana wamezaliana sanaaa.
mkuu acha unafiki na ubaguzi wa kanda.
Ni upuuzi kuzaliana sana ili eti mjulikane, Mbona watu wengi wanazijua Canada, Denmark, Norway, Urusi, Australi na Saudi Arabia na wako wachache??
Nigeria pia ni nchi ya kipuuzi sana ndio maana raia wake wengi wamekuwa matapeli na wauza dawa za kulevya kwenye nchi nyingine, hiyo sio nchi ya kupigiwa mfano.
 
Yoda atakwambia hao ni wanaharakati uchwara wa overpopulation.
 
mkuu iyo ni imani yako siwez kukubadilisha.lkn leta hoja za mantiki kwa wadau tuzijadili,sio ubaguzi unaoleta apa.
 
family planning fanya ww na familia yako,uko ume enda kwenye tamaduni za wahenga.hahaaa
 
Bila shaka wew ni mtumishi wa afya,kigoma hasa kibondo usiombe uwe upande wa kuhudumia watoto na wajawazito,mpaka unakosa muda wa kunywa chai

Sijui huwa nipoje siku za clinic nikionaga wamama wanaongozana na watoto wao mgongon naona ndo kama kazi ambayo wanawake wameshabakiza hapa dunian
 
Mimi nadhani tuisianglie kuzaliana bali tuangalie resources available, je hao Kigoma pamoja na kuzaliana vipi kuhusu resources ni under utilization au overutilization, kwangu tatizo sio kuzaa, tatizo ni hao wanaozaliwa wanakuwa liability badala ya Asset
 
Hili lingekuwa tatizo kubwa kama Kodi zetu zingetumiwa kuwahudumia wananchi, lakini sababu Kodi hizo hazitumiki kotoa huduma na ndio kwanza hawa watu wanatumika kukusanya mapato yanayoliwa utaona kwamba huo sio mzizi wa matatizo...

Tatizo ni kwa watunga Sera / Serikali kushindwa kutumia nguvu kazi iliyopo sio kwamba watu hawataki kupata ujira wao bali hakuna Sera za kuhakikisha watu hawa wanapata ujira...

Narudia tena tatizo la nchi hii na Afrika kwa ujumla ni corruption na ufujaji wa makusanyo.... (Watu, Siasa Safi, Uongozi Bora) sasa watu tunao siasa ni chafu na viongozi leaves a lot to be desired...
 
maskini kuzaa watoto wengi ni hasara tu na mara nyingi wanaishia kuwa maskini zaidi
 
Kama unatumia jembe la mkono na huna elimu ya kilimo hata uwe na ejari 1000 unakuwa ume underutilize resouces,so watoto ni luability sababu ya poor techn9logy and lack of capital to utilize resouces availabe
 
Hiyo kazi ya kuzaa wanaiujua sana hawa ndugu zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…