Mbona unauliza maswali ambayo hata mtoto mdogo hawezi kuuliza,kwamba wewe huoni miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na serikali yetu? Huoni uwekezaji mkubwa na wakihistoria uliofanywa na serikali hii katika secta karibu zote? Huoni namna vituo vya Afya vinavyojengwa kila Kona ya nchi yetu? Huoni hospitali za mikoa Kanda Hadi Taifa zinavyoboreshwa na kuongezewa uwezo wa kiviifaa na wataalamu ili kuweza kutoa huduma za kibingwa ambazo awali ilikuwa Ni mpaka mgonjwa apelekwe nje ya nchi?
Huoni uboreshaji wa secta ya Elimu? Huoni uwekezaji wa mabillioni ya pesa katika secta hiyo ambayo yamechochea hata ongezeko ya fursa za ajira kwa vijana? Huoni kwa Sasa Hakuna mwanafunzi anayekaa nyumbani kwa kukosa Ada au uhaba wa madarasa? Huoni kwa Sasa wanafunzi wote wanaripoti shuleni kwa wakati? Huoni kwa Sasa Elimu Ni bure Mpaka kidato Cha sita huku bajeti ya mikopo ya Elimu ya juu ikipaa Hadi kufikia billioni Mia sita na pointi? Huoni ukarabati na ujenzi wa shule mbalimbali kwote nchini unaofanywa na serikali ya Rais wetu mchapa kazi mama Samia?
Huoni mapinduzi katika secta ya kilimo? Kwamba hukusikia kuwa serikali imetoa mabillioni ya Ruzuku takribani billioni Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu?
Huoni namna mh Rais Rais alivyogusa maisha ya wakulima kwa uamuzi huo wa kizalendo na kijasiri? Huoni kwa Sasa namna kilimo kinavyowainua wakulima na kuwafuta wengi kujiongoza katika secta hii?
Huoni miradi ya bwawa la umeme na reli ya kisasa vikiendelea kwa Kasi nzuri? Huoni kukamilika kwa miradi hiyo inakwenda kulimulika na kuliangazia Taifa letu kila mahali? Huoni itachochea maendeleo ya viwanda kutokana na uwepo wa umeme wa uhakika? Huoni itapunguza Bei ya umeme na hivyo Bei ya bidhàa kuwa ya chini? Huoni kukamilika kwa rwli ya kisasa kutachochea usafirishaji wa bidhàa zetu na za majirani? Huoni bandari yetu ya Dar itapokea mizigo mingi na hivyo kuongeza mapato tutakayo wekeza katika secta nyingine Kama vile Elimu na Afya?
Kwamba hayo na mengi huyaoni? Kwamba wewe Ni kipofu? Au umetumwa? Au siyo mtanzania? Au unachuki binafsi na mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania mama Samia suluhu Hassani?