Mikopo kwa njia ya simu kilio kipya kwa Watanzania

Benki hawaangalii Hayo...wao wanachoangalia ni uhakika wa pesa yao kurudi...Sasa una dhamana mfano nyumba na mzunguko wa biashara mzuri watakuachaje ? Na tena wao ndio watakutafuta.
Sio kweli kuna kigezo kingine lazima waulize credit reference bureau kama wewe ni mdaiwa sugu sehemu yeyote ya mikopo iwe ya taasisi au online na uwezo wa kujua hilo wanao sababu hao wakopesha mikopo online nyuma yake kuna taasisi zilizosajiliwa kukopesha ndizo huendesha hiyo mikopo

Kipengele cha kwanza sasa hivi ukiomba mkopo kabla kuangalia vigezo vingine huanza kwanza kupata taarifa zako za ulipaji mikopo kutoka credit reference bureau na kujihakikishia kwanza kama wewe sio mdaiwa sugu popote ndipo waendelee na hivyo vigezo umetaja hawaanzii huko sasa hivi hiyo ni sehemu ya pili siyo ya kwanza kama zamani kabla ya ujio wa credit reference bureau

Dawa ya deni kulipa liwe la mkopo kupitia simu au online au popote kuepuka matatizo mbele ya safari

Wajinga wengine hutupa line akidhani akitupa line ya simu mkopo unafutika.na line aliyotupa haufutiki ng'oo laini ukisajili unasajili kwa kitambulisho cha taifa na dole gumba kitambulisho cha taifa na dole gumba popote vinabeba taarifa zako zote
Ukitupa line deni linazidi kukua tu na riba yake siku wakikuzukia watauza mali zako zote kufidia deni lao waweza kukufilisi kabisa
 
Hii ni hatari kwa wakopaji, yaani madeni madogo tu yamkoseshe mtu mkopo, dah!!

Itabidi tuhamie kwenye vikundi vya mtaani kama ndio hivyo, vipo vingi...kuanzia 1m hadi 5m unapata bila usumbufu.
 
Mkuu mimi nilinyimwa mkopo niliouomba kupitia crdb kisa deni la songesha!
Songesha mkopo uko chini ya Tanzania Commercial Bank wajinga hudhani ni mkopo wa line ya simu ya Vodacom ni mkopo wa benki ule wa Tanzania Commercial Bank zamani ikiitwa benki ya posta

Walichofanya kupunguza tu foleni kukopa watu wakope kupitia tu simu ambayo wameingia makubaliano lakini mkopo wenyewe huidhinishwa na benki yenyewe ukiomba
 
Na Mgodi ipo chini ya DTB, ukikopa hizi platforms ni kama umekopa Bank tu. Umakini ni muhimu sana.
 
Kupunguza foreni ya wateja wanao kuja benki kukopa 2000, 10,000, 50,000 100,000[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Hivi songesha inaweza kukukopesha 1m na zaidi?
 
Umeonewa tafuta ofisa mkopo alio nyooka, mkopo utapata faster tu.
Hata hivyo waliniambia nikajaze fomu, mimi tu nijafanya hivyo. Ina maana kwa watumishi huu mfumo wa ESS umeunganishwa na hizo system za kungamua wadaiwa sugar!
 
Na Mgodi ipo chini ya DTB, ukikopa hizi platforms ni kama umekopa Bank tu. Umakini ni muhimu sana.
Tatizo baadhi ya watanzania ujuaji mwingi anadhani akikopa online au pesa kwa simu basi huyo mkopeshaji bwege hajielewi anajitia ooh ananiķopesha mimi wakati hanijuì

Kumbe online wanaokopesha wanamjua vizuri kupitia line aliyosajili kupitia kitambulisho cha taifa na dole gumba lake

Mtu akitaka kujua kuwa wanamjua vizuri apoteze line aombe kurudishiwa line anaambiwa taja tu namba ya NIDA wataomba namba tu ya NIDA na dole gumba kila kitu cha taarifa zake hiki hapa
 
Mkuu sio ujuaji ni ushamba na umasikini, ukiwa na kitambulisho cha taifa huwezi kupotea popote, kama we ni mhalifu bora usijisajiri ta kitambulisho cha taifa, kabisa
 
Kupunguza foreni ya wateja wanao kuja benki kukopa 2000, 10,000, 50,000 100,000[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Hivi songesha inaweza kukukopesha 1m na zaidi?
Ni wewe tu una ongezewa viwango kadiri unavyokopa na kulipa wanakupima uaminifu wako tu

Wako watu wengi tu mbona akihitaji milioni sekunde tu mzigo unaingia na wako kibao mitandao yote tu milioni kitu kidogo mno cha msingi kuwa mwaminifu kukopa na kulipa .Huhitaji kupanga foleni kukopa benki au kujaza mikaratasi kibao na midhamana kibao kukopa milioni moja

Pesa kama hiyo ni kukopa simu kiganjani tu au online si ya kuzurura hata kwa ndugu kuomba

Simu zimekuja kurahisisha maisha kuna watu hawataki
 


Usikope! Naenda taratibu, wakati mwingine ukinyimwa Mkopo shukuru tu, hivi 30m riba yake ni kiasi gani? Utumwa huu Ndugu zangu, unaweza kukuza biashara taratibu tu bila presha pia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…