Mikopo kwa njia ya simu kilio kipya kwa Watanzania

Nikikumbuka niliwahi kupigiwa simu na kuambiwa nadaiwa na microfinance moja mtandaoni, jamaa nilipomwambia sina kitu nilisikia akicheka na kukata simu kumbe kucheka inaweza kuwa ndio taarifa zangu zilitumwa huko 😂😂
 
Wanajamvi habari zenu,

Kama kawaida nikikutana na kitu kipya lazima nikileta hapa kwa faida ya wengine. Ni kwamba wiki iliyopita nilikuwa nimeomba mkopo wa milioni 30 hivi kwenye mojawapo ya benki hapa nchini. Hii benki nimekuwa mteja wao tangu 2006 kama sikosei nimeshakopa kwao kwa zaidi ya mara tatu hii ikiwa ya nne. Ajabu ni kwamba, baada ya kufanya process zote za mkopo nilipigiwa simu nikaambiwa sitopewa mkopo kwa sababu mimi ni mdaiwa wa Sugu wa Mpewa nina deni la tangu mwaka 2020. Nilistuka kidogo lakini nikasema ngoja nifuatilie, hatua ya kwanza nilipiga simu Vodacom huduma kwa wateja kujua katika line zangu mbili za voda ni ipi ina deni?

Majibu kutoka Vodacom walinambia line zote hazina madeni isipokuwa kuna line moja likopa shilingi elfu 5 na ikawa muda wa kurejesha umepita. Hivo wakati deni linalipwa tayari taarifa zangu zilishaenda huko CRB kama mdaiwa Sugu. HII NI LINE AMBAYO ALIKUWA ANAITUMIA KIJANA WANGU CHUO kwa sababu wakati anaingia chuo alikuwa na miaka 16 kwa sababu alichagua kusoma kwa njia ya Cert, Diploma & Degree.

NI NINI CHA KUFANYA hili lilikuwa swali la pili. Jibu likawa kwamba nenda ofisi za vodacom zilizokaribu nawe ili upate ufafanuzi zaidi. Baada ya kufika Vodashop. Majibu ya Vodacom nenda NCBA Benki upate ufafanuzi zaidi. NCBA kwa official letter kabisa wakajibu hakuna deni na wakaonyesha tarehe ya mkopo na tarehe ambayo mkopo ulilipwa.

SWALI TENA NINI CHA KUFANYA KUCLEAR TAARIFA ZANGU HUKO CREDITINFO, jibu wapigie Simu, baada ya kupiga simu nikajieleza kisha nikaelekezwa kwenye Website yao ambapo nilijaza form ili kupewa taarifa zangu.
Majibu yalikuja ya ina mbili kwamba lile deni la Mpawa lilipwa lakini kwa kuchelewa hivo hizo taarifa zitabaki hivo kwa kipindi cha miaka sita tangu deni kulipwa.

MAAJABU SASA: Hata hii benki niliyokuwa ninaomba mkopo kwao nayo imeniorodhesha kama mdaiwa sugu kwa mikopo yote miwili ambayo yote nilishalipa nikamaliza. mkopo 2019 - 2022 na mkopo 2023 - 2024 ambayo yote imelipwa. Kwani baada ya kumaliza mkopo wa pili niliomba mkopo mwingine ambao ni watatu na sijafanya TOPUP.

Hili la benki nimefungua Dispute kupitia CRB ambaye ataawandikia ili wanijibu ndani ya siku 15 wakishindwa kufanya hivo nitakuwa huru kuwashitaki kwa Defamention. KUHUSU MKOPO WA BENKI NISUBIRI MPAKA MIAKA 6 IPITE.

Wasi wasi wangu ni kuwa kuna watu wengi sana ambao ama kwa kujua au kutojua huenda majina yao yako CRB na wako Blacklisted, kwa sababu kuna watu wamesajiri line za simu ambazo zinatumiwa na ama watoto, house girl, shamba boy nk. Katika hili nadhani CRB wangeangalia namna nyingine ya kurekodi taarifa wanazopokea kutoka kwa CREDITORS.

Mwisho nimenyimwa loan ya milioni 30 kwa sababu tu ya kucheleweshwa Deni la shilini elfu 5 ambayo iko chini ya NCBA.
Hatimaye nimeshinda Dispute yangu Creditinfo na bank wamenipatia mkopo kama nilivoomba
 
Me

Me pia niliwahi kuomba mwezi wa saba wakaniambia hivyo CRDB badae nikafuatilia nikaona wananilusha nikawaambia CRDB wanifutie maombi yangu ya mkopo kumbe walikuwa washapitisha makato mwisho wa mwez wakakata nikawapigia siku hiyo hiyo wakaniwekea changu chap so ongea na afisa wa mikopo tu chap
 
Back
Top Bottom