Mikopo kwa vyuo vikuu

Mikopo kwa vyuo vikuu

h.imani

Senior Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
189
Reaction score
94
NAOMBA UNIJIBU NA KAMA HAKUNA BASI FUATILIA HILI. Viongoji kwa mtazamo wangu wana ubaguzi wa hali ya juu sana, hii inamaanisha na serikali kwa jumla. '' watoto wa maskini na wa matajiri inatakiwa wapewe haki sawa kwenye ELIMU.

Sio tu Wanaosoma udaktari na wanaosoma ualimu ni watoto wa maskini bali hata wanaosoma masomo ya biashara, utawala nk. sasa ubaguzi huu utaisha lini?

Wanaosoma udaktari na ualimu wanalipiwa ada, tena ikiwezekana kwa 100% kisha ajira zao wanaandaliwa kabisa. Lakini wanao soma UCHUMI na biasha mikopo hawana na wanajisomesha na pia hata ajira zake hakuna''.

Sasa limu mtaacha ubaguzi huu? ILI CCM IENDELEE KUBAKI MADARAKANI BASI iache kabisa ubaguzi wa namna hii na kuhakikisha fani zote tunapata ngazi ya degree tunapata mkopo. Kila mtu afaidi matunda ya nchi kupitia viongozi wanaolitambua hili na sio ubaguzi, kwani kila mtu ana haki ya kunufaika na raslimali fedha za nchi hii kupitia ELIMU.
 
Mkuu umesema kweli kabisa ila nchi hii inatumia mfumo wa mwenye nacho anaongezewa na mwenye kidogo ananyang'anywa hata kidogo alichonacho.Ukifuatilia nchi hii haina kipaumbel cha dhati kwenye kuwapatia elimu watanzania.
 
Jamani sera ya elimu sehemu yoyote ile lazima iongozwe na mahitaji ya jamii yake, kwa sasa Tanzania ina mahitaji makubwa kwenye hizo kada japo kada moja ya ualimu hasa masomo ya arts huitaji umeisha.

Hivyo basi kutokana na ufinyu wa bajeti serikali inatoa kipaumbele kwa hizo fani na nyingine mnasoma kwa utashi wenu tu.
 
Hakuna cha udakitari wala nn hawa HESLB cjui wapo pale kwa maslahi ya nani mi niko bugando bachelor ya Medical Laboratory hadi sasa no bumu na kuna watu kibao hadi wa Md first year mkopo hausomi siyo uchumi na biashara tu ndio hawana bumu

na cha kushangaza tulibaniwa kupangiwa vyuo tulivyoomba mwanzo then baadae tukapewa vyuo hivyo hivyo tulivyobaniwa through transfer na tcu then walioenda vyuoni by transfer 90% mkopo haujasoma,

sasa kama mfumo wa transfer haukua na maana kwao si wangeacha tu ijulikane mtu kakosa alichotaka kuliko kuleteana usumbufu huu na vyuo vyenyewe vya afya ada yake ni mkasi.

Honestly wanaboa .......yaan niko tayar nikose pindi siku ya uchaguzi ili nikapige kura yangu may be utawala mpya utakuja na mapya.
 
Trichuris Trichura

Kumbuka tuliwatahadharisha mapema nyie mlioama vyuo kwamba kupata bumu huchukua muda mrefu lakini hamukusikia, haya sasa ngoja mnyolewe kwanza
 
Last edited by a moderator:
What i know bumu lake huchelewa kama ulikotoka ulikua tayari allocated ndio huchukua muda kuirudisha hela yako kutoka chuo cha kwanza kuja ulipo current sasa kama ulikua hujawa allocated huo muda wa kucheleweshewa bumu unatoka wapi, na kuna watu status zinasomeka NO LOAN usicomment usichokijua
 
Kumbuka tuliwatahadharisha mapema nyie mlioama vyuo kwamba kupata bumu huchukua muda mrefu lakini hamukusikia, haya sasa ngoja mnyolewe kwanza

Na utambue kwa chuo kama bugando kozi zote ni priority kwa swala la mkopo kila ukiwa katika moja ya kozi zinazotolewa kwenye medical school upo under loan consideration swala zinaingizwa politics hata sehemu zisizohusika
kama waliona transfer zinaleta shida wasingeimplement system kama hiyo inayotesa watanzania maskini
tuotion fee yenyewe CUHAS ni 4.3 millions siyo rahisi mkuu.
 
Budget exhausted inaniuma sana i can't forget and forgive them bora wangalisema hatuna hela na form watoe kwa idadi ya hela walizo nazo mazafantasaaaaaa hwa
 
Budget exhausted inaniuma sana i can't forget and forgive them bora wangalisema hatuna hela na form watoe kwa idadi ya hela walizo nazo mazafantasaaaaaa hwa

Hii ndio Tanganyika kwa style hii mtu unasoma kwa taabu hivi ada kubwa, no loan, mitihani unachezea belew za kutosha halafu uje umalize kwa mbinde then mtu akwambie uwe mzalendo.

fyuuuuu!!! huo uzalendo cjui utakua umekopeshwa na nani but one day tutafika wote tunakoenda
 
Back
Top Bottom