Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Mikopo kwa walimu, NMB vs CRDB

Ssayari

Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
16
Reaction score
8
Wanajamii, kwa wale wenye uelewa mzuri kuhusu hizi taasisi za kifedha,ni ipi hasa inatoa mkopo mzuri na kwa riba kidogo?

Swali lingine ni utaratibu wa paying off loan, yaani ulichukua mkopo baada ya miezi au miaka imepita ukapata pesa ukaamua kwenda kuwarudishia pesa zao Benki kabla muda wa kurejesha mkopo haujaisha,je,utalipa pesa yote uliyokuwa unadaiwa kwa kwa kipindi chote cha mkopo au kuna utaratibu gani?

Kashfa na matusi hakuna nafasi yake humu, nawaomba utaalamu wenu Great Thinkers.
 
Mwalimu Commercial Bank - MCB
imeanza. Je itakuwa mkombozi kwa waalimu. Je waalimu wakiamua kuitumia benki yao kutakuwa na athari kwa benki zingine? Ninajua kwamba hii bado ni benki mpya na bado haijaweka mtandao wake katika nchi nzima. Bila shaka macho yetu yako kwenye benki hii kama itaweza kuanzia pale ambapo zingine zimeishia.
 
Hii bank iunganishe mtandao wa saccos za walim nchi nzima..,
 
Riba za Crdb na NMB zipo sawa

Kuna jamaa Yangu alienda kuulizia ili apewe mkopo ambapo alianzia CRDB akaambiwa kwa mshahara wake anaweza kukopeshwa milioni 10 kwa muda was miaka 5 akaenda tena NMB akaambiwa mshahara huohuo anaweza kukopeshwa milioni 8.3 kwa miaka 5. Sasa inakuwaje mshahara huohuo mkopo utofautiane?
 
crdb inatoa mikopo mikubwa ila wana process ndefu hadi wakupatie.nmb wanamikopo midogo ila wanakupa ndani ya muda mfupi sana unaweza ukaanza process ndani ya siku tatu ukachukua mkopo. ukitaka mikopo yenye hela ndefu nenda EQUITY wanaweza kukupa hadi mil20 wanabranch yao mwenge na bagamoyo ila sijajua kwa mikoani.pia ukitaka kukopa inashauriwa nenda kakope mwezi wa sita maana benki nyingi huongeza viwango vya kukopesha.pia kama unataka kukopa bila riba unaweza kwenda kukopa PBZ ipo mtaa wa lumumba,karibu na ofisi ndogo ya ccm hapa dar es salaam,wanatoa mikopo mizuri hata kama mshahara wako unapitia kwenye benki nyingine ila wao hutaka wakukute kwanza kwa miezi mitatu ndo wakukopeshe unachotaka ukopeshwe.
 
Fafanua kwenye RED Mkuu
 
Fafanua kwenye RED Mkuu

mkuu utaratibu wao waliojiwekea ni kuwa kabla hawajakukopesha unachotaka kukopa,utatakiwa kwanza uwape marejesho ya miezi mitatu ya kiasi utakacho takiwa kurejesha kila mwezi.ukishamaliza miezi mitatu ndo wanakupa kile unachohitaji.nadhani kuna link yao ipo google nadhani unaweza ukagoogle na ukayapata maelezo ya kutosha mkuu
 
mkuu...unaongelea walimu wa mjini...asilimia kubwa wako mashambani...hizi benki zinaishia mjini...
nina ndugu zangu ni walimu na wengi wamechukua crdb kutokana na kuwa na riba ndogo..
kinachochelewesha ni uhakiki kutokana na walimu kupeleka taarifa feki.
 
mkuu utaratibu wao waliojiwekea ni kuwa kabla hawajakukopesha unachotaka kukopa,utatakiwa kwanza uwape marejesho ya miezi mitatu ya kiasi utakacho takiwa kurejesha kila mwezi.ukishamaliza miezi mitatu ndo wanakupa kile unachohitaji.nadhani kuna link yao ipo google nadhani unaweza ukagoogle na ukayapata maelezo ya kutosha mkuu
ukishapewa mkopo wanarudisha ilo rejesho au ndio imetoka?
 
nilienda kuuliza bank mbili juzi. nikaanza na crdb wakaniambia kwa salari yangu maximum watanipa 11,300,000 kwa miaka 6 na watanikata 257,000. nikaenda nmb wakaniambia maximum watanipa 9,500,000 na watanikata 251,000. Kimsingi hakuna tofauti za riba
 
Umesomeka vilivyo mkuu...shukrani!!
 
Tofauti ya riba ipo mkuu.,Hizi benk mbili Mikopo ya watumishi NMB ni 20% na CRDB ni,24% na mara nying CRDB watakuambia ni 20%..,kuna 4% huwa hawaionyeshi ila iko ktk makato ambapo 2% inakatwa kwenda PASS.,1.5 inakatwa kama gharama za mkopo.,na 0.5% hukatwa kama gharama za benk
 
CRDB wanaweza kopesha miaka 6?
 
Back
Top Bottom