Mikopo na sera mbovu za ubinafsishaji ndizo zimetufikisha hapa, Mwaka 2000 exchange rate ilikuwa(1 Usd=Tshs 803.3)

Unawezaje kukopa ukajengee vyoo vya mashuleni?

Shule ni huduma Si biashara,

Ulitakiwa tukope kuwezesha mitaji kwenye MABENKI yashusge interest rates za mikopo Ili watu wapate mitaji Uchumi ukue Kisha Serikali ichukue pesa kiduchu Toka faida kujenga vyoo,

Sasa kukopa ukaenda kujenga, huo Si Uchumi.
 
Kila mikopo inapoongezeka Thamani ya Dola inazidi kupanda😂😂
 
Nadhan Nchi hii kuna kakikundi ka watu wasiozidi 500 ndio wanaifaidi. PhD kibao zimefeli kuikomboa hii Nchi.
 
Hivi Wale wasomi serikali ya baba wa Taifa iliwasomesha bure kuanzia primary mpaka chuo
Walishindwa kusaidia uchumi wa nchi yetu ????
Mipaka Nyerere anatoka madarakani mwaka 1984,

Exchange Rate ya 1usd=10tshs

Mchango wa wasomi enzi ya Nyerere unaonekana.

Alipoingia Mzee Ruksa, ikashoot Toka 1usd =10tshs Hadi 1usd- Tshs 200+

Fungulia goli ndiyo imetutesa.
 
Very shallow analysis

Hakuna hata economic factor uliyoifanyia kazi

Shughulisha ubongo
 
Machawa hayawezi kusogea kwenye andiko hili
 
Soon pesa ya uganda inaenda kuwa na thamani kubwa kuliko yetu. Utasikia ush 1 = 1.7 tsh maana tunaporomoka hatari.
 
Soon pesa ya uganda inaenda kuwa na thamani kubwa kuliko yetu. Utasikia ush 1 = 1.7 tsh maana tunaporomoka hatari.
Hilo halitotokea ikiwa tutapata KATIBA mpya na Rais mpya 2025!!
 
Ni nchi ipi ambayo pesa yake imebaki vilevile bila kuporomoka dhidi ya dola tangu huo mwaka 2000?
 
Exchange rate si uchumi.

Mchina anapigana juu chini pesa yake isipande thamani. Anaifanya pesa yake iwe weak makusudi, isipande thamani.

Mpaka Mmarekani analalamika Mchina ana manipulate pesa yake iwe weak kwa makusudi.

Kwa sababu syrategy yake ni kuwa na weak currency ili ku promote exports.

Hata ukiwa na weak currency unaweza kuitumia kujenga uchumi mzuri.

Weak currency si tatizo, tatizo ni weak currency bila strategy.
 
Upo sahihi. Tena afadhali wawekezaji wa migodini ambao bidhaa wanazizalisha zinaingiza dola. Fikiria tunaleta muwekezaji anazalisha bidhaa anazouza humu humu ndani au anachezesha kamari. Huyu anatuuzia bidhaa kwa Tsh halafu anapopeleka faida kwao anazibadili kuwa dola na kuondoka nazo. Matokeo yake mahitaji ya dola na thamani yake inazidi kupanda na Tsh inazidi kushuka.

Ilitakiwa muwekezaji asiruhusiwe kuondoka na dola zaidi ya anazozalisha kwenye business yake au alizokuja nazo kama mtaji.
 
Ni nchi ipi ambayo pesa yake imebaki vilevile bila kuporomoka dhidi ya dola tangu huo mwaka 2000?
Majirani hawatuhusu,

Hiki ni kikao Cha ndani.

Tunaongelea Nchi yetu Tanzania. Unachotaka kusema ni kuwa, Jana tumelala njaa, lakini kumbe Si pekeetu, hata Jirani pia ni hivyo hivyo, Yeye alishinda uji, hivyo alituzidi kidogo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…