Na huu ndio ujinga ambao mimi huwa siuelewi. Kuna binti tulivutana hivi , ni pisi kali, na alikuwa anafanya kazi. Sasa nikamwambia njoo tuishi pamoja yaani unajua ile ya kulianzisha maana hakuna namna.
Nashangaa manzi anakwepa kwepa hilo swala. Yeye anataka awe na sehemu yake. Na alichonambia ni kuwa yeye anavitu vyake kwanza anataka afanye kwanza ili kutimiza ndoto zake sababu akiingia kwenye mahusiano ndoto hazitatimia.
Nikaona huyu kishalishwa sumu na mafeminist wacha nikaushe tu, maana mahusiano ya kulazimisha mtu ndio matokeo yake baadae mnaanza kusumbuana vichwa.
Tukawa tumebakia kuwasiliana tu. Mara ya kwanza nilichezea kirungu cha 100,000 mwaka jana 2022 mwezi wa pili akiahidi kunirejeshea miezi miwili ijayo. Hadi hapa ninavyoandika nadhani unakaribia mwaka sijaona hata mia ya ile laki yangu na kajikausha kimya haongelei chochote.
Mwaka jana huo huo kuna siku nilimpigia simu nikaongea nae akawa anashindwa kunambia tu ila alisema gesi imekata na anawaza hana mbinu. Nikajitoa kumwambia amwambie yule mleta gesi amletee kisha anambie nimtumie akafanya hivyo nikamtumia akasolve issue ya gesi.
Sasa tupo tu kwenye point hana cha kunambia na mimi namtazama tu kuwa kwa hizi akili kweli wanawake wa sasa ni mzigo kwenye maisha ya mwanaume.
Sasa wewe unaishi huko mbali na mimi nakuita uje tuunganishe nguvu tupambane na life wewe unakinzana halafu maisha yanakuzidi nguvu unataka mimi niwe nasimamia bill, huo ni upumbavu wa aina gani hivi jamani?