Mikopo ya benki ni wizi uliokomaa, nimetozwa riba ya 81% kwa miaka 6

Mikopo ya benki ni wizi uliokomaa, nimetozwa riba ya 81% kwa miaka 6

Unapewa milioni 20 , unalipa riba ya 81% kwa miaka 6. Je huu sio wizi uliokubuhu?
Wachumi tuelimishe is it worthy ta
Lakini si kabla ya kukopa mnaelimishana namna ya kulipa pamoja na riba husika? kama ni kweli sasa hapo sisi ambao hatukukopesha wala kukushawishi ukope tukusaidieje mkuu pamoja na uzi wako huu.

Dawa acha kukopa kopa bali pambana na hali yako kivyako vyako tuuuuu
 
Riba iliharamishwa kwenyr uislamu kwa sababu za msingi.
Ya kwamba mwenye nacho asimuexploit asiyenacho kwa sababu ya "shida" yake, enzi hizo watu walikuwa wanakopa kwa ajili ya shida tu kama chakula nk. Sku hizi pesa nayo ni bidhaa, inauzwa na kununuliwa, benki biashara yao ni pesa, wanapokuuzia wanataka faida, wanapokukopesha wanataka faida.

Mfanyabiashara anapokopa pesa naye anategemea akazungushe apate faida, sasa kwanini mwenye kukukopesha asitengeneze faida, pesa za kujiendesha na kukuza mtaji wa kuwakopesha wengine utamchangia wewe?!
 
Hiyo riba ni fair kabisa kwa kipindi hicho cha miaka 6.... hapo kwa mwaka mmoja inamaanisha ni 81/6 ambayo 13.5% (Hapo nime assume haijatozwa compound interest)

Hiyo riba hapo kuna mfumuko wa bei (Fedha kupoteza thamani) ambayo ni wastani wa 5% kwa mwaka, risk premium (Hii inafidia zile case ambazo mkopo haulipwi na benki ikapata hasara) kisha na gharama ya benki kwa ajili ya kulipia gharama za ku oparate
 
Kama hutaki kuibiwa, acha kukopa.
Njaa zako ndio zimekufanya ukakope. Hukushikiwa bunduki.
 
Unapewa milioni 20 , unalipa riba ya 81% kwa miaka 6. Je huu sio wizi uliokubuhu?
Wachumi tuelimishe is it worthy ta
Miaka inavyokuwa mingi na riba inaongezeka kwann usiulipe kwa miaka miwil tu au mitatu
 
"BENKI" gani hiyo ulikopa 20M ukarudisha 36M?!!! Maaana we ticha isijekuwa umekopa Bayport!
No, I am very smart. I just made an inquiry from a certain bank and was give that breakdown. I went into the loan calculator and confirmed that. By the way, I am not a teacher!
 
miaka inavyokuwa mingi na riba inaongezeka kwann usiulipe kwa miaka miwil tu au mitatu

Angalia kiasi ninachopashwa kulipa kila mwezi toka kwenye mshahara wangu. je mshahara unafika huko? Kama unafika kitabaki kiasi gani kulinda maisha ya kila siku


Loan amount: Num payments: Annual Rate: Monthly Rate: Monthly Payment:: Total Paid
20000000 36 .2200 .01833 763809.06 27497126.29


Total Interest:7497126.29


Loan amount: Num payments: Annual Rate: Monthly Rate: Monthly Payment: Total Paid:


20000000 24 .2200 .01833 1037563.0 24901514.2

Total Interest:

4901514.2
 
Hiyo riba ni fair kabisa kwa kipindi hicho cha miaka 6.... hapo kwa mwaka mmoja inamaanisha ni 81/6 ambayo 13.5% (Hapo nime assume haijatozwa compound interest)

Hiyo riba hapo kuna mfumuko wa bei (Fedha kupoteza thamani) ambayo ni wastani wa 5% kwa mwaka, risk premium (Hii inafidia zile case ambazo mkopo haulipwi na benki ikapata hasara) kisha na gharama ya benki kwa ajili ya kulipia gharama za ku oparate

Kama mkopo haulipwi benki wamekata bima
 
Juzi nimeenda benk moja kutaka milion 30, kwa miaka 5, nikaambiwa nitalipa jumla na deni milion 54, nikarudi nyumbani kunywa chai.

Crdb riba ni 20%, nmb riba ni 18% barclays 22%, bank abc 26% nk nk.

Hizi benk ni mufilisi. Riba kubwa sana.

Ila nadhani kama Magu ataendelea hivi watashusha maana walizoea kufanya biashara na serikali hasa kwenye hati fungani, serikali ilikua inalipa 15-16%, sasa inalipa 6%. Hawana namna watarudi kwa wananchi wa kawaida.
 
Sijapenda lugha yako, huwa nakuona mtu wa heshima hapa JF. Nakuweka kiporo! Sijapenda!
Pole kama nimetumia lugha kali. Kifupi mimi mwenyewe niliwahi chukua mkopo nikachanganya na pesa zangu. Nikanunua gari ya biashara. Ile gari haikumaliza mwezi bara barani ikawa written off. Since then ni miaka minne sujawahi kukanyaga benki kuomba mkopo kwa vile nilipata usumbufu mwingi sana toka benki juu ya marejesho. Nimeshaapa. Mtu akiniona nakanyaga benki kuchukua mkopo, anichinje kwa msumeno.
Kwa hiyo nikakuandikia vile (kwa lugha kali) nikutaadharishe kuwa kama hutaki kusumbuana na benki, achana na haya mambo ya mikopo.
 
Back
Top Bottom