Tayari nimeweka nia ya kutojihusisha na mikopo ya aina yoyote ile mwaka 2026. Iwe benki, viccoba au wowote ule nitakaa nao mbali. Yaani nimejiahidi kama nilivyojiahidi kutofanya mapenzi hadi nimalize form 6 na nikafanikiwa. Hii mikopo sio kabisa.
Kimsingi ukipiga hesabu ya marejesho ukajumlisha na gharama za uendeshaji wa biashara ni hakuna kitu mtu unafanya hasa mkopo unapokuwa wa benki. Ile mikopo ya kausha damu ya riba hadi 40% kwa mwezi sitaki kuitaja hapa kwa sababu ile ni kama kuamua kujiua kabisa. Hapa naongelea tu hii mikopo ya kawaida benki na VICCOBA.
Mimi ninashauri kama tupambane na tulichonacho mkononi huku tukiongeza nidhamu ya fedha tutafanikiwa. Stress za mikopo sio poa. Biashara ikiyumba tu kidogo benki wanapita na mtaji wako wote na isipotosha wanapita na nyumba, plot au dhamana nyingine uliyoweka. Wahanga ni wengi mno. Wengine hadi maisha wamepoteza.
2026 tuongeze nidhamu ya pesa huku tukikwepa mikopo. Ila ukipata ile mikopo ya CCM au halmashauri pita nayo.