Mshindi Nambari Moja
New Member
- Jul 14, 2021
- 1
- 2
Serikali kupitia bodi ya mikopo ya elimu ya juu hutoa mikopo (kwa riba) kila mwaka kwa vijana wanaofaulu ili kuwawezesha kupata elimu ya juu.
Binafsi naona jambo hili si sawa, kwani Elimu Ni moja kati ya haki za binadamu, hivyo haitakiwi kutolewa katika misingi ya matabaka yanayotengenezwa na "masharti ya kupata mkopo". Ni wajibu wa serikali madhubuti kuhakikisha kuwa raia wake wameelimika ili taifa liweze kunufaika na nguvukazi hii.
Vijana wengi ambao ndio wanufaika wakubwa wa mikopo hii, huamini kuwa, wakisha kuhitimu masomo yao wataajiriwa, hivyo kuanza kurejesha mikopo hiyo, Jambo ambalo halina uhalisia kutokana na upungufu wa ajira, hivyo vijana wengi hujikuta wakiishia kuwa tegemezi, huku wakiwa Ni wadaiwa sugu.
Takwimu zilizotolewa na nakala ya gazeti la Mwananchi ya tarehe 19.11.2019 zinadai kuwa, kati ya Novema 2015 na Desemba 2018, maombi ya kazi serikalini pekee, yalikuwa 594,300 wakati waliopata ajira Ni 6554 pekee(Tembelea www.mwananchi.co.tz)
Benki ya Dunia, inakadiria kuwa, takriban vijana 800,000 huingia kila mwaka katika soko la ajira Tanzania huku ñi 10% pekee ndio hufanikiwa kupata kazi.
Maswali ya msingi Ni Je, hawa wasio na ajira huelekea wapi? Hiyo mikopo huwa wanarejesha? Kwa namna gani? Kwanini nguvukazi ya Taifa inapotea bure kiasi hiki? Idadi ya watu inazidi kuongezeka, je, baada ya miaka 100 Serikali itaweza kutoa mikopo kwa asilimia ngapi ya wahitaji? Ni asilimia ngapi ya watanzania watapata haki yao ya msingi kwenye elimu?
Lakini, ukiangalia kwa jicho la Tatu, tatizo hili Ni matokeo ya "uminyaji wa haki za elimu" nchini.
Serikali imekwepa wajibu wa msingi wa kutoa elimu bure kwa watu wote na badala yake inakopesha elimu, jambo ambalo linawaongezea mzigo vijana, ambao walio wengi hawajawahi kukopa, hivyo hawajui namna ya kulipa hilo deni, na wakati huohuo hawana 'asset' za kuwawezesha kulipa hiyo mikopo. Kimbilio pekee ambalo hubakia kwao Ni ajira ambazo nazo pia 'zimeshakauka'
Ninaishauri Serikali mambo yafuatayo;
1. Serikali iache kukopesha elimu, ili kuwawezesha vijana wote wanaofaulu kupata haki yao ya msingi ya kuelimika na kutimiza ndoto zao.
2. Serikali itumie fedha ambazo hutoa kama mikopo, kuwekeza kwenye tafiti ' special project' ambazo hufanywa na wanafunzi. Tafiti hizi ziakisi moja kwa moja kile walicho kisomea. inaweza ikaongeza muda kidogo ili kupitia tafiti hzo wanafunzi watengeneze ama miradi, Taasisi ndogo ndogo, makampuni madogo madogo, viwanda vidogo vidogo au hata mashamba. Na hivyo vyote katika kipindi hicho, chini ya usimamizi, wazalishe kwa tija kwa kutumia elimu zao ili kupima uelewa wao. Mwanafunzi asitunukiwe shahada au stashahada yoyote bila kufaulu mtihani huu
3. Kama mwanafunzi atafaulu mtihani huu, maana yake utafiti huo umeleta tija. Maana yake kama Ni mradi Basi umezalisha kwa tija. Maana yake Sasa, serikali inaweza ikatengeneza sheria ili kuilinda miradi au viwanda hivyo, na wahitimu hao, hiyo iwe ndo ajira yao. Hapa Sasa wanaweza kuajiri vijana wenzao kwenye ajira zisizo rasmi, na hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kuajiri. Hivyo kadri idadi ya wasomi itakavyo kuwa inaongezeka, ndivyo uzalishaji wenye tija na wa kitaalamu utakavyo kuwa inaongezeka Nchini, badala ya kuongeza mzigo kwa serikali.
4. Serikali inaweza ikatoa muda maalum kwa vijana hao, na baada ya hapo itaanza kukusanya Kodi kutoka kwenye miradi hiyo, hivyo Ongezeko la pato la Taifa kwenda sambamba na ubora wa maisha ya watu.
Kadri wasomi watakavyo kuwa wanaongezeka, na ushindani pia utaongezeka, hivyo kuchochea Tafiti za masoko, na uboreshaji wa bidhaa na huduma. Hii inaweza kuchochea uuzwaji wa bidhaa zetu nje ya nchi kwa wingi na kutuletea pesa za kigeni.
Bila shaka, hii ndio maana halisi ya "ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA"

Upvote
2