Mikopo ya hazina, Maafisa Utumishi wanaomba 10% ili waweze kupitisha

Mikopo ya hazina, Maafisa Utumishi wanaomba 10% ili waweze kupitisha

Halmashauri zingine pesa zimetoka mda tu....mwezi wa 11, hakuna rushwa ya aina yoyote Ile....Mimi nimepata bila kumjua mtu halmashauri, nimejisajili hazina portal,nikapigiwa simu niandike barua nitumie kwa watsap,baada ya hapo....nikapigiwa simu nidownload mkataba, nimpelekee boss wangu asign, baada ya hapo nikawekewa mzigo...Tena walinipigia wenyewe kuwa mzigo umeingia. Huo ndio uzoefu wangu....kwetu hatujaombwa hata mia. Wenzangu waliniambia huo mkopo kupata hauwezi maana wanagawana wakuu wa idara tu.....nikawaambia kuwa hacha niombe Ili niwe sehemu ya ushuhuda wa haya mnayosema.....mwisho wa siku nimepata.
Umepata ngapi na ulichoomba ndicho ulichopata, maana nasikia waombaji mkiwa wengi mnagawana mkopo ilimradi kila mmoja apate kidogokidogo
 
Mwezi mmoja boss.....nimekunja mpunga wangu....mpunga Haina riba....unarudisha uliopewa....kifupi mshahara wako unapewa advance ya nusu ya mshahara wako....yaani unalipwa miaka SITA ijao nusu ya mshahara wako
Nshajisajil hazina na pal process za kuomb Zipo n kujaza na kusubmitt sasa Halmashauri yang ad sasa cjaon tangazo lolote je naweza omba nkafanikiwa kwa maana taarfa zkaenda kwa HR kimfumo?

Je ile sifa ya kuwa kupewa huu mkopo hutakiw kuwa na mkopo mwingine ipoje??
 
Wakikujibu naomba unitag na Mimi nahitaji kujua maana Nina kimeo nmb[emoji3064][emoji3064]
 
Wameweka sharti la 1/3 kuwaengua TGTS maana wanatajwa kuwa madeni mengi
 
Mwezi mmoja boss.....nimekunja mpunga wangu....mpunga Haina riba....unarudisha uliopewa....kifupi mshahara wako unapewa advance ya nusu ya mshahara wako....yaani unalipwa miaka SITA ijao nusu ya mshahara wako
Unavyosema nusu ya mshahara unamaanisha Nini?

Kama mshahara wangu ni 1m yaani laki 5 nalipa huo mkopo?

Au unachukua kiasi Cha mkopo gawanya kwa miaka 6 (miezi 72)?

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Kumekuwa na matangazo mbalimbali yanayohusiana na mikopo kwa wafanyakazi nadhani ni Tanzania Nzima.

Mfano kwa wilaya ya Uyui kuna 400, Tabora manispaaa kuna bilion 3, kwanza tunashikuru viongozi wa wilaya na mkoa kwa kutangaza mikopo hiyo kwani kuna wilaya ya nyingine na mikoa hakuna kabisa matangazo ya mikopo hiyo. Changamoto ya mikopo ni vishoka ambao ni maafisa utumishi na watumishi wengine wasiowaaminifu kwenye majukumu yao.

Mfano, nimeona tangazo la barua ya Tabara mjini watu waandike barua kisha wapate semina, hapo ndio Rushwa inapoanzia kwani kikawaida huwezi andika barua bila kuweka maji ya kunywa vinginevyo barua yako haitofanyiwa kazi. Pia Rushwa ya ngono itatawala kwa wadada kwani ikumbukwe mikopo hiyo haina riba.

Mikopo wafanyakazi wameambiwa waombee hazina portal, watu wajisajili kisha waombe, na wakishaomba mikopo italipwa kupitia Mishahara yao na makato yataingizwa na maafisa utumishi kulingana kiasi kitachoombwa.

Sasa hii ya kuitana na kuanza kupeana semina ni ulaji mwingine ambao viongozi wanautengeneza. Wafanyakazi wamekuwa wanachukua mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha na hazijawahi kutoa semina.

Kinachofanyika mkoa wa Tabora ni kutengeneza mazingira ya Rushwa kwa sababu barua haziitajiki katika maombi haya.

Nimeona pia Uyui wamewaambia watu waombe kupitia hazinal portal lakini anayehusikana kuingiza makato amekuwa akipigiwa simu hapokei tangu tangazo litoke na pia anajuzingusha kukutengenezea mazingira ya ile 10% ambayo lazima iachwe.

Serikali imekuwa ikifanya jitihada za dhati kututoa katika analojia kutupeleka katika digital kupitia mifumo yake mingi ambyo imeianzisha mfano "EES" salary slip portal na nk. sasa tusirudi kwenye mambo ya kuandika barua kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunapingana na serikali.Tanzania ni yetu sote

View attachment 2842864View attachment 2842867View attachment 2842869
Mkuu barua ya pili uliyoweka iko Classified as Confidential, siyo poa kabisa. Lkn kweli unakopesheka weka salary slip yako tujue nani mwenye shida wewe au hao Viongozi wako.
 
Mkuu barua ya pili uliyoweka iko Classified as Confidential, siyo poa kabisa. Lkn kweli unakopesheka weka salary slip yako tujue nani mwenye shida wewe au hao Viongozi wako.
mbona unabwabwaja? confidential nini?! mbona hayo mabarua yapo watasap
 
Mkuu barua ya pili uliyoweka iko Classified as Confidential, siyo poa kabisa. Lkn kweli unakopesheka weka salary slip yako tujue nani mwenye shida wewe au hao Viongozi wako.
wapi imeandikwa kama confidential?
 
mbona unabwabwaja? confidential nini?! mbona hayo mabarua yapo watasap
Sawa Nurse endelea na mtindo wako wa Maisha uliyochagua kwenye Utumishi. Am sorry kukushauri. Nimefuta kauli uko sahihi kwa kila jambo.
 
Hiyo mikopo ina magumashi sana Maafisa huko wilayani hawatoi ushirikiano na mara nyingine hawatoi kabisa taarifa sahihi.

Kwa mfano:

Wilayani Maswa tuliambiwa tuombe kupitia mfumo wa advance loan salary ( ALS) sasa kilichotokea kumbe huko wilayani wakaamua pia watu waombe kupitia barua bila kutoa taarifa yeyote kuja kushtuka deadline imefika. Hivyo wamepeana wenyewe hiyo mikopo.

Nini kifanyike...

SERIKALI IBORESHE MIFUMO WATU WAOMBE KWENYE MFUKO BILA HATA KUONANA NA HAO NGURUWE HUKO WILAYANI...
Naungana na wewe kwenye hoja ya kuimalisha mifumo. Kiukweli hivi vijamaa vinayoitwa afisa utumishi kwa baadhi ya maeneo ni kero tu. Hivi vijamaa ni kama vimesomea kuomba rushwa na kama kweli elimu waliyoipata ndio hiyo basi kwa sasa vingi vina PHD ya kuomba rushwa na kupiga tarehe wateja wao wanaowahudumia.

Lakini bado nashaka na hili la mifumo maana ninaona baadhi ya vipengele vinawahusu hawa maafisa utumishi na kuendelea kwao kuhusika yawezekana vikaja kusema mifumo ni usumbufu na kuishauri serikali kuifuta ili viendelee na system ya upigaji wanyonge.
 
Shida sio halmashauri, Ni hazina wenyewe, kwa nini wasitangaze kuwa kuwa kuna mikopo, waorodheshe halmashauri zote fedha zilizopo na masharti ya kupata na deadline, hii mikopo Ipo miaka mingi Ila nauhakika 90% ya watumishi wa umma hawajawahi kuisikia, Ni kakundi ka watu kanajitangazia na kujikopesha
 
Nshajisajil hazina na pal process za kuomb Zipo n kujaza na kusubmitt sasa Halmashauri yang ad sasa cjaon tangazo lolote je naweza omba nkafanikiwa kwa maana taarfa zkaenda kwa HR kimfumo?

Je ile sifa ya kuwa kupewa huu mkopo hutakiw kuwa na mkopo mwingine ipoje??
Mpaka watoe tangazo halmashauri Yako....kujisajili jambo Moja na halmashauri Yako kuingia mtandaoni ni jambo lingine
 
Back
Top Bottom