Ndugu zangu mikopo sio kitu kibaya, na kwa kampuni kubwa au nchi mikopo ya maendeleo hulipwa kwa muda mrefu. Kwa individual kukopa then ulipe kwa miaka 20 sio rahisi maana nguvu zinakuwa zimeanza kupungua.
Ila kwa nchi, kukopa leo, kuna kizazi ambacho kinafaidika na mkopo sasa na msingi wake uwe wa kuifanya Tanzania ya leo na kesho iwe na neema na matumaini kuliko tusingekopa.
Rais yangu kwa wakubwa ambao wana dhamana ya kukopa kwa niaba yetu ili baadae sisi na wanetu tulipe, kopeni ili riba ya mabenki ya uwekezaji kama TIB na TADB ishuke na masharti ya mikopo kwa start-up investment projects yawe na fursa ya kuwafanya Watanzania wakope sio kama individuals ila watengeneza kampuni za kuzalisha bidhaa na huduma.
Miezi kadhaa imepita nilikuwa naongea na mtu mmoja alifanya kazi serikali ya mchonga, Mzee Ruksa na BWM, nyakati zile Tanzania ilikuwa ina-export wastani wa marobota laki 6 kwa mwaka. Victoria federation enzi hizo ikiwa na ofisi ya mauzo ya Pamba London.
Leo mauzo ya pamba, bila shaka haifiki hata robobota laki 1, maana yake uzalishaji umeshuka..
Kwanini TADB na TIB wasije na investment projects loans ili kampuni za Watanzania ziwekeze kwenye kilimo cha kibiashara kwa ku-mechanize mashamba yawe na mfumo wa umwagiliaji, pamba ivunwe, kampuni zingine ziundwe zikopeshwe textile machinery ili Tanzania iuze nyuzi, vitambaa hata nguo, ili hao wanetu ambao leo 1.3Tril inajenga madarasa yao, in 15 years wawe na sehemu ya kufanya kazi kwenye viwanda vya mnyororo wa thamani wa Pamba.
Hii ikihusisha kuwa na kampuni zingine zinazalisha mbolea na all the agro-chemicals ili hela ya imports ya agro-inputs ibaki ndani izunguke kwa ku-service deni.
Kwanini Tanzania isiwe exporter wa nyama middle east kwa kutumia advatange ya ng'ombe tulionao? Kwanini Tanzania isiwe exporter wa leather products baada ya kuwa tumechakata ngozi za ng'ombe?
Akina Ng'wigulu wataalamu hapo wizarani ya fedha, fikiriene kuifanya agro-commercial projects, dunia ina watu bil 7, tuuze walau SADC all the basic consumables.
Itakuwa aibu kama tutakopa pasi kujenga financial instrument itakayo-stimulate uzalishaji ambao utavutia forex.
Tanzania based on the vast of resources, tusipojiandaa kwenye uwekezaji wa miradi ya kibiashara, ipo siku zile projects za Nyanzaga Gold, Mahenge Graphite na gas ya kusini ziki-peak na kuna fursa ya kuuza kuku laki 1 na mayai say laki 3 kwa siku, tutabaki tunashangaa wakati nchi ndogo kama netherlands yenye idadi ya ng'ombe wachache kuliko Tz, ila kwa kuwa na ubora wa uwekezaji kwenye agribuz, wanauza nyama, mayai, maziwa na kuvuta forex ya kutosha kuliko sisi.
In 2019, the Netherlands exported €94.5 billion worth of agricultural goods. That is a 4.6% increase on the €90.4 billion export figure for 2018.
In 2019, the Netherlands exported €94.5 billion worth of agricultural goods. That is a 4.6% increase on the €90.4 billion export figure for 2018. Around two-thirds of this growth is due to an increase in export prices, while a third is due to higher export volume. Last year saw not only an...
www.government.nl
Dunia ya sasa mauzo ya agri-process ni biashara kubwa sana. Kwanini hatuna mauzo ya sausage from fresh water.
Hela toka kwenye mzunguko huo itasisimua makuzi ya service sector kama lega, insurance, banking, logistics, consultancy just to mention a few;
€90.4 billion ni sawa na TZS 247Tril.
Assume Watanzania tuwe na kampuni zenye mauzo ya wastani wa 20% ya nini Uholanzi walipata na TRA ika-tax hizo biashara, nchi ingepata kiasi gani?
We need the gov. to setup a room availability of financial instrument for Tanzania owned corporations to invest in know-how, technology and hire experienced expertise to make a game change in agri-investment.
Agribuz bado hatujagusa hata 5% ya potential ya nchi hii; ila kama ni kilimo cha kufa na kupona na kutegemea kudra za Mwenyezi ambacho ndicho kilichopo, basi; itapita miaka 20, Tanzania itaendelea ku-import toothpick, chupi, leso, toilet paper, gundi, penseli, chaki vitu ambavyo could be made in Tanzania.
Tunaomba kupata platform ya ku-dialog na madam SSH ili tufanye mambo haya yatokee.