JMF
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 1,758
- 2,770
Moja kwa moja kwenye mada,
Mwezi June nilipokea sms kuwa kuna jamaayangu kaniweka kama mtu wake wa karibu na amekopa pesa ameshindwa kurejesha. Nilishtuka sana, nikapiga kujua ni milioni ngapi kumbe ni elfu 25,000. Baadae jamaa nikamuuliza akacheka, akanieleza ni mikopo ya online ila atawarejeshea weekend. Ndipo nami nikawajua na nikawakopa Tsh17,000 wakanipa kwa siku nane na riba ni Tsh300.
Siku ya saba wakanitumia sms mfululizo kama 20 hivi kuwa nilipe mkopo haraka. Nikapotezea sababu siku ya nane bado. Siku ya nane saa kumi na moja hata sijaamka wakaniita tapeli. Nilikwazika sana, nikaweka 20,000 nakuwalipa 17,300. Nikapokea sms kuwa bado nadaiwa kama 8400. Nikaingia kwenye App yao ya Cash-X nikakuta nadaiwa bado elfu nane na zaidi kama service charge.
Nikasema hawa siwalipi. Wakamtumia sms yule jamaa yangu (yule aliyenitonya kuhusu hii hao pesa x) kuwa wananidai. Hapo zinakuja sms kama mvua toka namba zao mbalimbali nyingine za kejeli na matusi juu. Nikawalipa hiyo 8400 ikiwa ni siku ya kumi na moja. Nimelipa nikapokea tena sms kuwa bado nadaiwa kama 1500 eti ni penati(adhabu) kwa kupitiliza muda wa mkopo.
Nikasema acha nimalizane nao ila malipo ni hapahapa bongo. Baada ya mwezi wakanitumia sms kuwa wameniongezea kiwango cha mkopo hadi 50,000. Nikasema sasa acha niwanyooshe hawa wahuni. Nikakopa nikaenda kunywa bia na yule jamaa yangu kupunguza hasira. Leo ni mwezi wa pili wametuma sms, kutukana na kukejeli hadi wamenyoosha mikono juu.
Jamaa walimtumia sms akawambia simjui huyo mtu. Nimewaambia nilipo, waje wanikamate wanipeleke mahakamani ili nami niwafungulie kesi ya kunitukana