Mikopo ya Pesa X, Cash X au Singularity Microfinance ni kausha damu

Mikopo ya Pesa X, Cash X au Singularity Microfinance ni kausha damu

JMF

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
1,758
Reaction score
2,770
Moja kwa moja kwenye mada,

Mwezi June nilipokea sms kuwa kuna jamaayangu kaniweka kama mtu wake wa karibu na amekopa pesa ameshindwa kurejesha. Nilishtuka sana, nikapiga kujua ni milioni ngapi kumbe ni elfu 25,000. Baadae jamaa nikamuuliza akacheka, akanieleza ni mikopo ya online ila atawarejeshea weekend. Ndipo nami nikawajua na nikawakopa Tsh17,000 wakanipa kwa siku nane na riba ni Tsh300.

Siku ya saba wakanitumia sms mfululizo kama 20 hivi kuwa nilipe mkopo haraka. Nikapotezea sababu siku ya nane bado. Siku ya nane saa kumi na moja hata sijaamka wakaniita tapeli. Nilikwazika sana, nikaweka 20,000 nakuwalipa 17,300. Nikapokea sms kuwa bado nadaiwa kama 8400. Nikaingia kwenye App yao ya Cash-X nikakuta nadaiwa bado elfu nane na zaidi kama service charge.

Nikasema hawa siwalipi. Wakamtumia sms yule jamaa yangu (yule aliyenitonya kuhusu hii hao pesa x) kuwa wananidai. Hapo zinakuja sms kama mvua toka namba zao mbalimbali nyingine za kejeli na matusi juu. Nikawalipa hiyo 8400 ikiwa ni siku ya kumi na moja. Nimelipa nikapokea tena sms kuwa bado nadaiwa kama 1500 eti ni penati(adhabu) kwa kupitiliza muda wa mkopo.

Nikasema acha nimalizane nao ila malipo ni hapahapa bongo. Baada ya mwezi wakanitumia sms kuwa wameniongezea kiwango cha mkopo hadi 50,000. Nikasema sasa acha niwanyooshe hawa wahuni. Nikakopa nikaenda kunywa bia na yule jamaa yangu kupunguza hasira. Leo ni mwezi wa pili wametuma sms, kutukana na kukejeli hadi wamenyoosha mikono juu.

Jamaa walimtumia sms akawambia simjui huyo mtu. Nimewaambia nilipo, waje wanikamate wanipeleke mahakamani ili nami niwafungulie kesi ya kunitukana
 
Hiyo mikopo haifai na ina makato mengi ambayo hauambiwi kabla... Kuna dada amekopa 20000, baada ya kupewa anapaswa aje arejesho tsh. 26000+1000 ya ada ... hapo hujaweka hela ya kutolea wala ile utakayokatwa wakati wa marejesho...


Mwisho unakopa 20000, kwa kazi gani? Mikopo ya chap chap iogopeni bora taasisi rasmj za kifedha hawana uhuni na makato yaliyojificha fichA.
 
Niliwakopa 10000 nilikarudisha 16000 wakanipa 195000 nikapotea [emoji16][emoji16][emoji16]
Hawa wahuni hawataweza kudumu kwenye soko, watapotea siku siyo nyingi. Tatizo lao nikwamba wameajiri vijana wahuni ambao hawajui biashara. Riba yao(wenyewe wanaificha kwenye kichaka cha kuiita service charge) nikubwa sana halafu ikitokea bahati mbaya mteja akipitiliza tuu siku1 waanze kutukana, kukejeli na kutuma vitisho huku wakiongeza adhabu kwenye mkopo. Wasipojirekebisha watafunga virago mapema sana
 
Mara ya kwanza nilikopa Premier Cash 20000 lakini nilipokea 16000 na inabidi nirudishe 24000

Sijawahi kopa tena.
 
Hawa wahuni hawataweza kudumu kwenye soko, watapotea siku siyo nyingi. Tatizo lao nikwamba wameajiri vijana wahuni ambao hawajui biashara. Riba yao(wenyewe wanaificha kwenye kichaka cha kuiita service charge) nikubwa sana halafu ikitokea bahati mbaya mteja akipitiliza tuu siku1 waanze kutukana, kukejeli na kutuma vitisho huku wakiongeza adhabu kwenye mkopo. Wasipojirekebisha watafunga virago mapema sana
Mimi waliponitukana tu ...nikawaambia Asante kwa kunitusi silipi. Mpaka leo hawajaribu
 
Dawa yao ni App ya SHOULD I ANSWER? Hakuna namba ngeni inakupata bila idhini yako, so unaweka hiyo App kila wakipiga ni inatumika miaka na miaka tu.
 
Back
Top Bottom