Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 262
- 361
Hellow JF.
Leo nimeamua kukusogezea hili, Ivi sasa familia nyingi sana zimekuwa zikipitia mazingira magumu sana ya kuhangaika,kuteseka,masimango,mates na Madhira mengi saana. Wengi wanaishia kupambana na changamoto hizo bila mafanikio na wengine wanaishia kufurukuta Kadri wawezavyo lakini matokeo Yanabaki kuwa yale yale, mateso/Mahangaiko mfululizo...
Sasa katika utafiti wangu mdogo nimegundua familia nyingi zinazopitia mazingira haya ni zile ambazo Kuna mateso au masononeko miongoni mwa viongozi wa familia mfano, Baba au Mama.
Jamani turudi nyuma kidogo, hata ukisoma au kuskiliza maneno ya wazee wetu wamekuwa wakitusisitiza kwamba BABA na MAMA ndio miungu wa hapa duniani. Hii maana yake kwamba watu hawa wanaweza kuwa Baraka au mikosi katika maisha endapo mmoja wapo atakengeuka na kuwalea watoto katika misingi ya kumdharau yoyote miongoni mwao. Familia nyingi za kileo zilizogubikwa na kila aina ya masaibu au mateso mbalimbali ya dunia utakuta mzazi mmoja kajiona yeye ndio muweza wa yote,mkamilifu na anaepaswa kuskilizwa yeye tu ambapo hutumia muda mwingi kueleza mabaya ya mwenzake kwa watoto hatimae watoto hao kujikuta wanamdharau mzazi mmoja na kumpuuza kabisa, hali ambayo hupelekea maumivu makubwa saan kwa mzazi mwingine.
Hali ambayo inapelekea mzazi huyo kuumia ndani ndani kwamba mtoto wake wa kumzaa anamdharau au kumpuuza kiasi icho.
Na hapo ndipo mikosi huingia katika familia ama kizazi, manung'uniko au maumivu ya mzazi mmoja hupelekea mikosi kwa watoto kiasi ambacho hakuna kitu watoto hao watafanya kizae matunda hata wafanye nini. Itakuwa ni kilio,lawama na majanga kila kukicha.
Njia ya kuondoa mikosi hii.
1. Kila mzazi achukue nafasi yake- acha kabisa kueleza watoto wako changamoto za mwenza wako,mlikutana wawili na mkapendana wawili Vumilia.
2. Watoto lazima wawaheshimu wazazi wote NI LAZIMA, na mtoto ukiona mzazi yoyote anakueleza mabaya ya mwenza wake- pale pale mueleze kwakweli hayo hayanihusu,( mwambie nakushauri muyazungumze maaana nyie wote wazazi wangu na nnawapenda wote)
3. Tujitahdi sana kufata utaratibu mzuri wa kupata mwanamke anaeweza kuwa Mama na Mwanaume anaeweza kuwa BABA. Zingatia sana hili, maana kosea vyote usikosee kuoa au kuolewa.
4. Mungu ndio kila kitu- kila unapowaza kufanya jambo fulani muweke Mungu mbele, yeye atakufunulia njia njema ya kumpendeza na isiyo na matatizo yoyote.
Mwisho, Mikosi mingine haitoki kwa walimwengu, mingine tunaitengeneza wenyewe tuiepuke bila kurudi nyuma.
Karibuni kwa maoni🙏