Mikutano iliyotangazwa kufanyika nchi nzima na Katibu Mkuu CCM siyo mikutano ya hadhara iliyozuiwa na Rais?

Mikutano iliyotangazwa kufanyika nchi nzima na Katibu Mkuu CCM siyo mikutano ya hadhara iliyozuiwa na Rais?

Mbogo nyeusi

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
233
Reaction score
541
Najiuliza Kama katibu mkuu CCM ametangaza kufanyika mikutano ya hadhara nchi nzima itakayo fanywa na wabunge, madiwani, wenyeviti wa CCM wilaya,kata,vijiji na mitaa,zuio la Rais lilikuwa linawahusu watu gani?

Pia Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM naye anazunguka kiaina kukutana na wananchi na anajibu hoja za washindani wenzake Kama mwenyekiti wa chama CCM, je hafanyi mikutano ya hadhara aliyoizuia yeye mwenyewe?

Sababu ya kuzuia mikutano ya hadhara kwa vyama vingine vya upinzani ni zipi na chama tawala kujifanyia mikutano chenyewe kina hofu gani? Kama chama wanazunguka kujiimarisha kwa nini wazuie wengine kwa kutumia dola wao wasijiimarishe?

Alipo Rais kama wenyekiti wa chama CCM huwa pia wapo wenyeviti wa mkoa,wilaya na hata viongozi wengine kitaifa na wanachama waliovalia sare za chama, je hiyo siyo nafasi ya mwenyekiti wa CCM anaitumia kuimarisha chama?

Je, hiyo mikutano iliyo agizwa na katibu mkuu wa chama CCM kufanyika na wabunge wa CCM madiwani na viongozi wengine watakuwa hawavai sare za chama?

Kwa huu uonevu ipo siku utatugarimu Kama taifa kila chama kina haki sawa kwa mujibu wa katiba,je CCM wanaogopa wapinzani kwa kuwa viongozi wake hawana uwezo wa kujibu hoja jukwaani?

Ni aibu mwenyekiti wa CCM kuzuia wenyeviti wa vyama vingine kufanya mikutano ya hadhara kwa uoga wa kushambuliwa majukwaani,

Hoja ya kwamba mikutano inarudisha uchumi nyuma,je hao watu watakao hudhuria kwenye hiyo mikutano iliyo agizwa kufanyika nchi nzima si wataacha kazi zao na kuhudhuria hiyo mikutano? Je, hapo hawajarudisha uchumi nyuma kwa huo muda wanaoenda kusikiliza viongozi wao?

Ni vyema tuambiwe ni jinsi gani mikutano ya hadhara inaharibu uchumi na kurudisha maendeleo nyuma lakini ilifanywa na wanaccm inapaisha uchumi juuuuuu!!
 
utamzuiaje mwenye nyumba kutembelea mashamba yake? huwezi kumuachia nyani azungukie maana utakuta mabua pumbafu hawo cdm
 
Aliyempa nyumba na hayo mashamba nani?Jamani tupeleke watoto wetu shule waweze kufanya uchambuzi (analysis) wa mambo.
hata nyie mkiwa na utawala hamuwezi kumuachia mtu mwingine awaangalizie himaya yenu lazima muangalie wenyewe mbuzi nyie
 
Suluhisho nikupeleka mswada wa sheria bungeni kuondoa kazi za vyama vya siasa,tuna sheria ambazo zinaamriwa na MTU mmoja.HAKUNA HAKI
 
Wakafanye Mpaka MBINGUNI ikiwapendeza.

JamiiForums-1005591240.jpg
 
Wabunge wameruhusiwa kufanya mikutano majimboni mwao..
.
.
😀😀
 
Vyama vya upinzani andaeni mikutano, watu wahudhurie. Heshimuni katiba na sheria. Puuzeni kauli za kibaguzi za Mwenyekiti wa CCM za kuwaruhusu CCM kufanya mikutano na kuwazuia wengine.
 
Back
Top Bottom