Mikutano iliyotangazwa kufanyika nchi nzima na Katibu Mkuu CCM siyo mikutano ya hadhara iliyozuiwa na Rais?

Mikutano iliyotangazwa kufanyika nchi nzima na Katibu Mkuu CCM siyo mikutano ya hadhara iliyozuiwa na Rais?

Kila chama kiitishe mikutano sehemu kiliposhinda tu. Japo CCM tulishinda sehemu zote. Poleni UKAWA.
 
Kila kitu mnalalamika! Muwe mnasikiliza vizuri yanayoongelewa ili kuepusha aibu ndogo ndogo kama hizi.
Mimi nadhani kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa rasmi, hakukuwa na sababu yoyote muhimu ya kuizuia. Katiba inaruhusu, na ilitamkwa bayana baada ya Sheria ya vyama vingi vya siasa, kuwa mikutano hiyo ya hadhara inawekwa kwenye Katiba ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kuizuia. Kimsingi, mikutano hiyo ni moja ya kazi muhimu zinazotakiwa kufanywa na vyama vya siasa ili kutangaza sera zake na hatimaye kupata Wanachama.
 
Sasa kama wewe ulisikiliza vizuri ukaelewa kuna ubaya gani ukawaelewesha wenzio hapa ambao hawajaelewa?
Wabunge/Madiwani,wenyeviti wa mtaa,wafanye mikutano ktk maeneo yao, Mwambie mbuge wako haitishe mkutano,alafu amwalike katibu au Mwenyekiti wako mfanye mkutano
 
Wabunge/Madiwani,wenyeviti wa mtaa,wafanye mikutano ktk maeneo yao, Mwambie mbuge wako haitishe mkutano,alafu amwalike katibu au Mwenyekiti wako mfanye mkutano
Kwa kifungu kipi cha Katiba/sheria ya JMTZ?
 
Kwa kifungu kipi cha Katiba/sheria ya JMTZ?
Ni vyema vyama vya upinzani waende mahakamani tuone mahakama itaamua nini kulalamika tu hakusaidii chochote,Kama hawana pesa ya kufungua kesi mahakamani tujulishwe tuchangie
 

20210629_011921.jpg
 
Uwezo wa uelewa wa Tz kidogo umeongezeka, hivyo Ccm lazima iogope Uhuru wa kusikia na kuchambua hoja hadharani. Mikutano ya wapinzani ni mkuki mchungu sana kwa CCM na watawala kwa ujumla. Ukiruhusu mawazo huru, itakuwa mwisho wa CCM na watawala kwa ujumla.
Binafsi nilijua kuwa huyu mama anahatarisha maisha ya CCM kama ataruhusu haki ndani ya nchi hii.
Style ya ukandmizaji ya mtangulizi wake ndo njia pekee ya kuinusuru CCM. Nafikiri hill wamemnasihi wala kwa mgongo wa CCM wenzie, na sasa inabidi afanye hivyo bila ile hofu ya Mungu aliyo anza nayo.
Ila binadamu hakawii kusahau yaliyo mtokea mwenziwe, je anajua kuwa Mungu yupo likizo?
 
Back
Top Bottom