Pre GE2025 Mikutano ya CHADEMA yadoda Vunjo

Pre GE2025 Mikutano ya CHADEMA yadoda Vunjo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika operesheni ya siku 21 ya kukijenga chama hicho kanda ya Kaskazini inayoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Ndugu Freeman Mbowe imekutana na mahudhurio hafifu sana Jimbo la Vunjo, Moshi DC mkoani Kilimanjaro.

Hali hiyo imepelekea Mwenyekiti wa kanda hiyo wa chama hicho anayemaliza muda wake Ndg Godbless Lema kuwafokea wananchi kuwa wanawavunja moyo kwani kazi hii wanayofanya ni ngumu na wanajitolea hivyo kutojitokeza kwenye mikutano kunawavunja moyo viongozi.

Katika mikutano yao katika kata za Kahe na mji mdogo wa Himo mikutano ya chama hicho kilipata mahudhurio hafifu licha ya helikopta waliyokuwa nayo kuzunguka raundi tatu angani kabla ya kutua ili kufanya hamasa.

Wengine walioonekana kwenye ziara hiyo ni pamoja na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Vunjo Grace Kiwelu ambaye aliachwa na mume wake wa ndoa Ndg Sindato Ndesamburo Kiwelu baada ya kukosa uaminifu kwenye ndoa.

View attachment 3037995
View attachment 3037996View attachment 3037997
INASIKITISHA WALLAH.
 
Hayo mambo ya watu wengi au wachache ni ujinga tu. Kinachotakiwa ni dhamira ya kila mmoja, kuelewa ccm si chama kitakachotuletea maendeleo na kutoa umasikini. Kimeshashindwa kwa miaka zaidi ya 60.
Hilo jimbo chadema wanalichukua mapema tu , yule bwana kimei huko amechacha inasemekana lakin🤔
 
Hilo jimbo chadema wanalichukua mapema tu , yule bwana kimei huko amechacha inasemekana lakin🤔
Hili jimbo lipo neutral, ajaye awe ni mwenye akili kubwa na mtendaji, kimei ameshindwa kukaa na wanajimbo kindugu, kutatua shida nje ya mifumo ya serekali, nikimaanisha kushirikisha wananchi naye akiwepo kujenga mabarabara na mengineyo, wachaga by nature hawakuzoea KUILILIA SEREKALI KAMA SEHEMU ZINGINE ETI KWA KIGEZO TUNALIPA KODI, WACHAGA HUITATUA KERO KWA NAMNA YOYOTE KWANZA!
 
Back
Top Bottom