Mikutano ya teuzi za CHADEMA kwa ajili ya uchaguzi 2020 kutokuwa live kwenye mainstream media: je, chama kiliomba na kukataliwa au hakikuomba kabisa?

Unaomba tu?😁! Wamekuwa walemavu?

Hata mvua yenyewe inaombwa masika siyo kiangazi!

Kila siku ITV wanawatangazia wanasiasa wakalipie kupata coverage walianza na kipindi cha MREJESHO ikaja sijui kipindi gani sikikumbuki.

Ujamaa ulishajifia kibudu kitambo mazee!

The Wailing Wailers!
 
Jibu ndo hilo ACT ni programu ya Chama tawala kupunguza nguvu ya Chadema so wao kuoneshwa live na channel zenu uchwara ni moja ya mipango mikakati ya CCM kuua nguvu ya Chadema

Kwa hiyo chadema walikwenda kuziomba media zika kataa? Chadema hebu semeni ukweli
 
We simama uhesabiwe wenyewe wataunga tela uwepo wa Mungu ni zaidi ya hizo media zote 2020 tunaenda na mpango wa Mungu 2020 ni yeye ni Lisu

Kwa hiyo wagombea wengine hawana Mungu? Hebu jibu maswali ya msingi kama ulivyo ulizwa....
 
Chadema wanashindwa kulipia airtime wakitegemea huruma ya wenye media sasa kwa hali ilivo mifukoni sioni mmiliki wa chombo cha habari atakubaliana nao. Kila mmoja ale alikopeleka mboga. Kwa ukata walio nao wataendelea kuonekana "Chadema in blood" tu kule insta
 

Mkuu weka ushahidi kama hakuna vyombo vilivyo hudhuria na jinsi vilivyo tishiwa....
 
Huwa vinalipiwa, siyo bure. Tena bei zake ni kubwa kwa saa! CCM iliweza kulipa media zaidi ya tano 24 hours for 4 days. ACT wamemudu kulipia media moja (ITV) kwa saa moja.
Chadema wameshindwa kabisa kwa kwa sababu ya ukapa!
Who are you to tell Chadema what to do?
 
Pointi yako nimeilewa sana.
 
Wewe unaamini ACT ni upinzani kweli??
Sio upinzani how comes mnafanya nao mazungumzo kupeana support? Huu ubinafsi wa kishamba kujifanya nyie pekee ndo unaujua sana upinzani na kuforce kila mtu awatambue kama role model wa mabadiliko ndo inawashusha na kuonekana chama cha kiharakati kisicho na dira yoyote ya msingi..
 
Utakuja kuelewa badae. Hata nzi akiacha ujinga anaweza tengeneza asali. Kuna muda puppets huwa wanabadirika kikubwa kwenda nao kiakili
 
Kama kuna mtu humu anaweza kukumbuka kilichowakuta marehemu Mzee Mengi na Spencer Lameck Lumumba kwenye kukabidhiwa cheti cha ushindi. Waliokolewa waziri Membe. Walishambuliwa mawe, viatu na kila kitu. KISA ?! Ni kwanini ITV na radio one walikuwa fair ktk uchaguzi mkuu 2015 . Ni kwanini waliiwatangaza Cdm ?!. Mwisho waliishia kupigwa fine za kutosha na kutishiwa kufungiwa.

Juzi tu jumapili DW walikuwa na kipindi. Lakini kina RFA walikata matangazo yaliomhusu Lissu . Sasa ndiyo watangaze mkutano mkuu ?!. Serikali za ki communist ni shida
 
Hawa jamaa hawako serious ndo maana hata ukiwatag hawajibu pamoja na kuwa na account humu tena verified.
 
Hakuna chombo chote cha habari ambacho kiliripoti siku lissu amekuja nchini?? Huu uongo huwa mnaupendea nini? Vyombo karibu vyote viliripoti
Nakuwekea hapa chini
 
Watu wanasema jf kuna GT lakini si kweli na haijawahi kuwa kweli.
Mtu anaongopa kitu ambacho watu wanaweza kabisa ku-prove, lakinj hawafanyi hivyo badala yake wanakubaliana nae tu
Ilikuwa kuna ugumu gani watu kupita you tube au IG au twitter kuona kama kweli vyombo vya habari viliripoti au laa
Hawa jamaa hua ni walalamishi tu hamna unachoweza kuwafanyia wakashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…