Dr Msaka Habari
Member
- Apr 9, 2022
- 66
- 32
Akiendesha program kwa wadau mbalimbali waliofika kuchangia jana Dar es Salaam mmoja wa wawezeshaji wa mada Jane Msigita amesema uchumi jumuishi wa kaya baadhi ya wanawake wanaweza kuwa hawajui kile ambacho wanachangia hali inayopelekea mwisho wa siku wanakuwa hawatambuliki katika mchango wa kaya.
"Mila potofu hazichangii uchumi jumuishi hazina nafasi katika uchumi endelevu ," amesema Misigita.
Msigita aliwataka wachangiaji kuchangia mada hiyo kwa upana kwa kulenga fursa za shughuli jumuishi katika jamii.
Aliongeza kusema kuwa katika kulenga shughuli hizo jumuishi ata katika sehemu nyingi za masoko shughuli nyingi zenye fursa zimekuwa zijifanywa na wanaume.
Naye afisa program mwandamizi mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) zainabu mmay amesema kuwa usawa wa jinsia,desturi,mitazamo,imani ni kikwazo pekee cha kufikia uchumi jumuishi na maisha endelevu.
Ameongeza kuwa pamoja na mambo hayo jamii imeelezwa kuna uwezekano wa maisha ya wanafamilia kama taasisi za kindoa kuishi vibaya na kusababisha malezi mabovu kwa watoto.