Milion 10 inatosha kuanzisha biashara ya Baa?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Milion 10 inatosha kuanzisha biashara ya Baa? Uzuri wa biashara hii unaweza fanya popote budget yangu ni mil 10 ambayo itajumuisha TV 3, friji, viti, meza, jiko, wafanyakazi 3 wa kuanzia, mziki mkubwa (sijui bei yake) ingependeza kama kuna watu wanafanya biashara waje watoe uzoefu wao.
 
Kabla hujafanya biashara yoyote ile ni lazima uijue hiyo biashara kwa kufanya utafiti, wapinzani wako ni wakinanani nguvu zao zikoje mapungufu yao, wateja wao ni wakinanani na wanapatikana wapi, wewe nguvu zako na mapungufu yako wateja taraji, utakabliana vipi na upinzani uliopo na ujao kwakifupi ni lazima uwe na andiko la biashara.

Pia mzuki mkubwa siyo lazima inategemea eneo la biashara na aina ya wateja kwa eneo husika (audience) lapili ni sifa za wahudumu (sifa za mjasiriamali), traits, angalia pia biashara zingine km hiyo muunekano upoje kwasa na hapo baadae itakuwa vipi, (market trends)
 
Kabla hujafanya biashara yoyote ile ni lazima uijue hiyo biashara kwa kufanya utafiti, wapinzani wako ni wakinanani nguvu zao zikoje mapungufu yao, wateja wao ni wakinanani na wanapatikana wapi, wewe nguvu zako...
Uzoefu ninao wa kunywa tu wa biashara ya bar sina. kuangalia washindani wangu hili nitalizingatia lakini pia kwasababu sina uzoefu itabidi nikae kaunta angalau mwezi mmoja then ndo niweke mtu.
 
Hiyo siyo budget mkuu na simaanishi kukuharibia siku yako ila achana na hiyo biashara huiwezi.
 
Uzoefu ninao wa kunywa tu wa biashara ya bar sina. kuangalia washindani wangu hili nitalizingatia lakini pia kwasababu sina uzoefu itabidi nikae kaunta angalau mwezi mmoja then ndo niweke mtu.
Kama huna sifa hata moja kati ya hizo za wajasiriamali huwezi kufanya biashara yoyote, mimi ni muelimishaji elimu ya ujasiriamali kwa vitendo na pia naandika kitabu cha ujasiriamali, ambacho utakisoma unakiweka kwapani unaanzisha biashara, (simama dede), karibu
 
Zinatosha sana Bora kuanza biashara ndogo yenye makosa kidogo nirahisi kuyajua ,kujifunza na kuyarekebisha
Hapana, biashara lengo lake ni kupata faida.

Na kama ukitulia kidogo na kufanya utafiti, utapata faida. Pia siyo lazima uanze na kitu kikubwa, unaweza kuanaza na biashara ndogo na ukaikuza.

Kwa mfano grocery au Lounge ndogo yenye waitress mmoja na kibox cha chips na mishikaki au mchemsho asubuhi (hata kwenye hotpot tu).

sasa badala ya kuongea blabla hebu tuonyeshe jinsi unavyoweza kuanzisha "Bar" kwa milioni kumi.
Tuonyeshe bajeti ya mahitaji, matumizi ya kila siku/mwezi na income 9expected).

Tuanze hapo kwanza.
 
Hapana, biashara lengo lake ni kupata faida.
Na kama ukitulia kidogo na kufanya utafiti, utapata faida. Pia siyo lazima uanze na kitu kikubwa, unaweza kuanaza na biashara ndogo na ukaikuza...
Nina mpango wa kuandika hiyo template ambayo itakuwemo kwenye kitabu changu, but at my own time after conducting a. Market research within my mapping area as a reference in my book, hapa tunajaribu kuelimishana not showing off that we are more knowledgeable than others
 
Sasa kama hujawahi fanya huo utafiti, au huna experience ya hiyo biashara, kwanini unatoa ushauri?
 
Mkuu mambo vipi,

biashara ya bar inategemea na unataka kuiweka maeneo gani na unataga wateja wako wawe watu wa aina gani. ila kwa mtaji wa million 10 unaweza kuanza kwa maeneo ya nje kidogo ya mji kama ni hapa dar es salaam.

pia kama utahitaji vitu kama TVs nzuri na muziki nicheki mimi nitakupa kwa bei nzuri ya jumla pamoja na warranty ya uhakika..

kwa ushauri wa bar ninao pia ila sema kwanza unataka hii bar iwe maeno gani ndio upate ushauri
 
Sasa kama hujawahi fanya huo utafiti, au huna experience ya hiyo biashara, kwanini unatoa ushauri?
Unatatizo kichwani yaani mimi nianze kuandika template hapa km unataka naweza kukukuandikia dodoso ili ufanye utafiti, mimi ni muelimishaji elimu ya ujasiriamali na nimebobea kwenye eneo Hilo hata hiyo biashara nimewahi kufanya , Hiyo biashara inarudisha uwekezaji wako ndani ya miezi 6 km utaifungua kwa kishindo, (with a big bang)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…