Milioni 200 zajenga madarasa Ludewa, kamati ya siasa yapita kukagua

Milioni 200 zajenga madarasa Ludewa, kamati ya siasa yapita kukagua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MILIONI 200 ZAJENGA MADARASA LUDEWA, KAMATI YA SIASA YAPITA KIKAGUA

Ikiwa tunaelekea mwezi Januari mwezi ambao wanafunzi huripoti shuleni kuanza na kuendelea na masomo yao, kamati ya siasa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imefanya ziara ya kukagua vyumba 10 vya madarasa katika sekondari mbalimbali vilivyojengwa hivi karibuni kwa fedha zilizotolewa na serikali kuu kiasi cha sh. ml. 200.

Katika ukaguzi huo kamati hiyo ilijigawa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza lilielekea ukanda wa mwambao na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wa wilaya hiyo Stanley Kolimba huku kudi la pili likiongozwa na katibu wa chama hicho Gervas Ndaki sambamba na wakuu wa idara mbalimbali na hapa wanatoa kauli yao baada ya kukamilisha ukaguzi huo.

Joseph Kmonga ni mbunge wa jimbo la Ludewa lakini pia ni mjumbe wa kamati hiyo ya siasa amesema ili kuboresha majengo ya serikali na hasa katika uwekaji wa vigae kuna haja ya kuwakusanya pamoja mafundi na kuwapa elimu.

Aidha kwa upande wake katibu wa siasa na uenezi wa wilaya hiyo Josaya Luoga sambamba na afisa elimu sekondari Mi kael Hadu ambaye alimuwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya Ludewa walikuwa na haya ya kusema.

Ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa unaenda kupuguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuendelea kuboresha majengo yaliyo mengi ambayo yameonekana kuwa machakavu kutokana na kutumika kwa muda mrefu.

IMG-20230109-WA0029.jpg
IMG-20230109-WA0032.jpg
IMG-20230109-WA0033.jpg
 
Back
Top Bottom