Milioni 22 ninunue gari ninayoipenda au nichukue IST kwanza? Sijawahi kumiliki gari

Milioni 22 ninunue gari ninayoipenda au nichukue IST kwanza? Sijawahi kumiliki gari

Achana na IST chagua moja kati ya hizi;
1. Toyota Kluger
2. Crown Athlete
3. Benz c class
4. BMW 3 series
5. Rav 4
6. Harrier
 
Kaka nisikilize,
Kama hujawahi kabisa kumiliki gari ya kukuchangamsha akili. Nunu brevis 6mil hizo zinazobaki zitakupa uzoefu wa spea na mafuta.
Ist itakulemaza akili.
Brevis unataka kumuua mwenzio kwa Pressure Bora aendelee na mpango wake wa IST hizo hela nyingine akahonge tu
 
Nunua kitu roho inapenda
Kikubwa uwe na taarifa sahihi mf kuhusu matumizi,garage nzuri nk na utunze gari lako
 
Kuna mtu amekupa ushauri mzuri sana kama utaamua kuufuata
Ni hivi; Kununua gari sio shida sana , tatizo ni GHAHARAMA ZA KILA SIKU ZA UENDESHAJI hii hubadilika kutokana na Eneo ulilopo ( Umbali unao tembea kila siku na Aina ya Barabara kama lami au Vumbi)
Mfano: Umejipanga kutumia kiasi gani kwenye gari kila mwezi (laki mbili, tatu, nne au Laki tano?)

IST inatembea wastani wa KMS 14- 17 hivi kwa lita; Rav 4 na familia nyingine za aina hiyo (around cc 1750 -2000) inatembea wastani wa KMS 10 - 12hivi kwa Lita
Ungetujibu hayo maswali ungeweza kushauriwa vizuri
 
Back
Top Bottom