Milioni 4 inatosha kufungua biashara ya grocery au duka la pombe kali?

Milioni 4 inatosha kufungua biashara ya grocery au duka la pombe kali?

Hey, wapendwa

4M inatosha kufungua grocery?

Kama inatosha je vitu gani muhimu?

Na yenyewe inatakiwa kuwa na Vibali au unaweza kufungua kama duka la mangi?

Nafikiria kwenda field ili nipate uzoefu

Yaani niombe kazi hizo sehemu zinazouza pombe, sijuh ni grocery au ni bar.

Ili niweze kufahamu 1,2,3

Kama unafahamu kuhusu hii business basi naomba nipewe uzoefu.
Kauze maembe
 
Kama we mzuri na una lugha laini hata 2 inatosha kwa liquor shop
 
Ila grocery ni duka la kuuza mboga mboga na matunda nadhani hili hata kwa ml 2 unafungua tena la kisasa kabisa Cha msingi upate wauza mboga na matunda wazuri wawe wanakuletea na uwe na fridge zuri
 
We should not fear life just because it has twists and turns! Uoga wetu ndio umasikini wetu.
No my point is reminds him how hard it takes to be businessman we have to fall many times before being successful in what we do so we should never give up even if we fail many times.
 
Just remember 9 out of 10 bussness fails during 5 years of business so expect it.
Consistency ndo inafelisha wengi,, watu sio wavumilivu wanataka mafanikio ya haraka, nidhamu ya pesa nayo ndo sababu ya business kufa maana mtaji unakata mapema biashara inafungwa.
 
Sina uzoefu sana na hio biashara lakini kuhusina na watu wanaojishughulisha na hio biashara wengi ninaofahamiana nao mtaji wao hakuna alie zidi milioni tatu.
Wewe anza uzoefu na ujuzi utaupata baada ya kuanza.
Iwe heri kwako.
Wewe unaongelea pub hizi za mtaani
 
Wanaosema inatosha sijui wanatumia hesabu gani.sasa hivi kreti za soda Pepsi na coca cola kwenye gari ni elfu kumi na Tano hapo hazina maji yake.

Kreti za bia kununua kwa agent wa tbl ni elfu kumi na tatu.kwa agent wa sbl ni elfu kumi na mbili mia Tano hapo hazina maji yake.Sijajua Kwa maeneo utakayokuwepo

Shelf hujatengeneza Bado hujanunua pallet.hujaenda TRA,manispaa,cheti cha TBS,mashine ya EFD na vyeti vya afya Kwa wafanyakazi vinahitajika viwepo, vinapatikana Kwa bwana afya Kwa njia mchongo bila ya hivyo kila mara watakuja kukukagua.

Bado hujalipa Kodi ya fremu.hujanunua thamani za ofisi kama meza na viti.

Matumizi yote hapo juu Bado hujakuwa na bidhaa ya kuuza ili uingize pesa.hapo umepaki pesa ambayo haizalishi.
Bado hapo unatakiwa uache hela ya emergency hata 1M incase, hio pesa haitoshi
 
Wanaosema inatosha sijui wanatumia hesabu gani.sasa hivi kreti za soda Pepsi na coca cola kwenye gari ni elfu kumi na Tano hapo hazina maji yake.

Kreti za bia kununua kwa agent wa tbl ni elfu kumi na tatu.kwa agent wa sbl ni elfu kumi na mbili mia Tano hapo hazina maji yake.Sijajua Kwa maeneo utakayokuwepo

Shelf hujatengeneza Bado hujanunua pallet.hujaenda TRA,manispaa,cheti cha TBS,mashine ya EFD na vyeti vya afya Kwa wafanyakazi vinahitajika viwepo, vinapatikana Kwa bwana afya Kwa njia mchongo bila ya hivyo kila mara watakuja kukukagua.

Bado hujalipa Kodi ya fremu.hujanunua thamani za ofisi kama meza na viti.

Matumizi yote hapo juu Bado hujakuwa na bidhaa ya kuuza ili uingize pesa.hapo umepaki pesa ambayo haizalishi.
Inatosha kabisa kufungua grocery..
1.Mtaji wa vinywaji milioni moja na nusu
2.viti, meza, friji ndogo, naksinakshi milioni moja na nusu
3.Pango miezi sita na mengineyo milioni moja, huitaji efd
 
Back
Top Bottom