Milioni 70 inatosha kufungua Pharmacy ya jumla jijini Dodoma?

Mil 70?
Frame akibahatika chini sana hiyo30 imeisha...
Mnapenda kutisha watu jamani frame 30M??

Nilipata frame kwa mwezi 1M na ilikua location nzuri

Nikapata connection MSD ingawa ukienda kichwa kichwa hawatoi dawa mpk kwa mawakala wao

Angalizo: ni biashara inayohitaji usimamizi sio Unaishi Mbeya duka kkoo
 
maximum frem atalipia laki tano kwa mwezi hadi laki mbili na nusu kwa chini sasa piga mara 12 au x miezi 6 mkupuo. ila matengenezo ya ndani kuanzia shelves za kipharmacy (sio za kiduka la dawa muhimu) na maboresho yoote, haipungui 10 - 15. bado matengenezo kwa nje kama ubao wa tangazo la uwepo wa pharmacy (digital), bado hajaweka akiba ya kulipa wafanyakazi si chini ya wawili watakaopokezana kwa zamu, na pia, kama wewe sio mfamasia jua sio chini ya 1m utakuwa unalipia cheti cha mfamasia kukitundika pale. iliyobaki ni mtaji, manake yeye anasema ni duka la jumla.
 
Frame hakuna kkoo ya kuuza dawa za jumla kwenye lile eneo utapata kwa laki tano.

Mkuu dawa hazina bei hiyo 70M inatosha trust me!!!
 
Watu wanapenda kutisha watu frame kkoo bei za ajabu,
Ila ukienda bei ni 300-1000k

Tena nzuri tu, ukiwa mtu wa maneno unampanga mwenye frame anakupa kwa miez 6
 
Mil 70?
Frame akibahatika chini sana hiyo30 imeisha...
Nyinyi ndo hamjawahi kua kwenye game, hapo kkoo nilikua napaogopa ila nimeingia kwenye game uhalisia ni tofauti kabisa Yani, frame za milion 30 kwa mwaka na vilemba ndio zipo, ila hata za milion 15 kwa mwaka zimejaa tele sana mpaka zinamwagika
 
Mtaji kariakoo kwa wastani ni sh ngapi?
 
Mtaji kariakoo kwa wastani ni sh ngapi?
Milioni 70 kando kando ya mji ni nyingi tu na jumla unafanya na faida kubwa unapata.

Changamoto ni pale kiriakoo ukiingia kichwa kichwa unaweza kuumia. Maana ushindani wake sio haba

Kimsingi fanya utafiti kwanza wa mazingira na machimbo ya kupata dawa kwa bei nafuu kabla hujaanza hiyo biashara ya jumla.
Best of luck
 
Hahahahahaha we jamaa hutaki Tsh 50m monthly? Hiyo environment unayoenda itakupa 50m per month? Acha kuleta ujanja hapa.
 
Daah tutafika lini sijui idea za biashara tunazo mitaji hatuna. Kukopa tunakwamba hatuna dhamana.

Yote kwa yote hongera, kuna stage ukifika ni ya kujipongeza.
Share hizo idea na sisi tuzione kama nzuri ili siku tukipata hela tujilipue
 
Kafungue kariakoo halafu uza Jumla hiyo hela inatosha, Dodoma haitokulipa mzunguko mdogo naongea kwa uzoefu.

Pharmacy jumla kariakoo inalipa ndo maana sasa hivi wakina Robby One wakina Vunja wako huko!!
Aiseee.
Kafungue kariakoo halafu uza Jumla hiyo hela inatosha, Dodoma haitokulipa mzunguko mdogo naongea kwa uzoefu.

Pharmacy jumla kariakoo inalipa ndo maana sasa hivi wakina Robby One wakina Vunja wako huko!!
 
Mkuu simara naomba ni dm please naona ume lock dm nashindwa kukutumia message
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…