Millard Ayo amejifunza nini kwa kilichotokea kwa mfanyakazi wake mpiga picha kufariki

Millard Ayo amejifunza nini kwa kilichotokea kwa mfanyakazi wake mpiga picha kufariki

Sijui kwanini mifumo ya hosp haijaunganishwa na mifumo ya polisi. Ilitakiwa ukifika pale kama ni ajali unapokelewa unahudumiwa na pale pale hosp pawe na namna ya kuwapatia taarifa polisi kuwa tumepokea majeruhi, au Pale pale hosp getini kuwe na dawati maalum na polisi mmoja kwa ajili ya hayo mambo.
Ukiachana na hili la mfumo bado dharula yoyote inayohitaji matibabu inatakiwa ikimbizwe hospitali, mgonjwa atapatiwa huduma ya kwanza bila kujali ni raia mwema au jambazi kisha hospitali itawajibika kuwasiliana na polisi.

Hivyo emergency room zote zinapaswa kuwa na namba za wakuu wa vituo walio karibu nao.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh

Kweli.
 
kwenye ile ajali ya boda na ist,dereva wa boda ndio alipata majeraha makubwa sana maana yeye ndiyo alikuwa mbele mwili wake kukutana na ile dhoruba moja kwa moja na ndio maana boda boda wakaona wamuwahishe kwanza yeye maana ndio alikuwa na hali mbaya zaidi eneo la ajali ila kwa bahati mbaya alienda fia hospitali baada ya siku kadhaa.
Ndugu mwandishi kwa kuwa alikuwa abiria inaonekana yeye aliumia zaidi ndani na baada ya ajali alikuwa anaongea kabisa na kujitambulisha kazi yake na ndio maana wakasema asubili msaada wa polisi lakini ya Mungu mengi kumbe jamaa kukaa chini kwa muda mrefu na kutopata huduma kwa wakati ndio ikapelekea kifo chake pale pale na watu hawakutegemea kwa sababu yeye hakuumia kama alivyoumia yule boda.
 
Back
Top Bottom