Millard Ayo: Bilionea mstaarabu

Millard Ayo: Bilionea mstaarabu

-Ayo TV ni ya nani?
Kuna online TV,yenye nguvu Tanzania kuzidi AyoTv?
 
5M USD ni zaidi ya 10B za Kitanzania! Anashindwa nini kuanzisha Radio Station yake?? Ili awe free zaidi na kufanya kazi zake yeye mwenyewe?? Kipindi kama amplifier anachofanya pale Cloud's akihamishie kwenye Radio yake na apige pesa nyingi zaidi??
Hizo ni mbinu zako za kibiashara, na yeye ana zake pia. Nenda kamshauri.
 
Ndiyo maana nikauliza hilo swali! 5M USD ni parefu sana! Hizo pesa sio la mchezo eti! Unaweza omba leseni Central Bank,ukaanzisha Bank yako!

Hahhaaa,,kwanza fobes yenyewe huwa siwaamini,,,
 
Labda Bilionea wa kibongo kuwa na nyumba na gari ndogo,ila ubilionea wa US BAADAE SANA.
 
Mbona hutuambii jamaa anaoa week ijayo??
 
Mimi pia nilitaka kujua hilo, kwanini aendelee kuwa mtumwa wa mtu wakati ana uwezo wa kutosha kufanya yake na kuajiri zaidi na zaidi...?
Sio formula hiyo mkuu,,
Niliwai kuskia interview moja ya big joo anamzungumzia milard nadhani wana mutual agreement and understand,
Mwenyew anakubali kua millard anaweza kua anaingiza pesa nyingi zaid yake.
By the way millard ana studio kubwa tu na wafanyakazi wengi sana anawalipa..
Nafkiri ka target sana online radio,tv na content kiujumla huku akitumia clouds ku keep his name alive kifupi yeyewenyew ndio brand na anajua anachokitafuta kwenye yale masaa mawili anayotangaza pale clouds na inamlipa sana..
 
Kivipi social network ziwe mali ya clouds?
Amplifier ni ya clouds
Youtube labda inawezekana sina uhakika kwa ufahamu, lakini hapo kwenye twitter ig na fb naomba nifahamishe
Sababu zimekuzwa kwa kutumia rasilimali za Clouds. Bila Clouds wewe ungejua kuna mdudu anaitwa Ayo? Wakienda mahakamani wanamshinda mchana kweupe, ni kama mume atake kuacha mke bila kumpa chochote wakati ulichuma ukiwa nae, hata kama wewe ndio uliingiza pesa yote na kununua vitu vyote bila mke kutoa hata mia, bado anahaki na kila ukichopata ukiwa nae, labda kama alikukuta navyo na Vikabaki katika kiwango kile kile bila kukua ukiwa nae.
 
Hiyo haiwezi kuwa sababu millard ayo waiati anaenda clouds alitoka radio one ambayo ilikuwa imeiacha mbali sana clouds.
Clouds ataacha kipindi cha ampifaya tu
Ayo wa Radio one na wa Clouds ni sawa? Huwezi kuacha mke bila kumpa stahiki zake kwa ulivyopata ukiwa nae. Kila kitu ataacha hapo, popote mahakamani anapigwa mueleka asubuhi na mapema. Konde boy alilipishwa bilioni kadhaa kubaki na account zake alipotoka wasafi, hizi media Groups sio wajinga...!
 
One of the richest bloggers in Africa Forbes ilinukuu.

Ukimuona simple tu wa kawaida lakini ana hela ndeefuuu na nyingi sana.

Utajiri wake unakadiriwa 3-5 Millions US dollars. Vyanzo vingine vya uhakika na kuaminika vinadai anaweza kuwa na utajiri hata zaidi ya iyo dollar million 5.

Ni kwa kujituma kwa Millard na weledi alionao umemfikisha hapa alipo. Ana mchango mkubwa kwenye taifa kwa kutoa ajira hasa kwa vijana na kulipa kodi.

Ubunifu wake na kujituma kwake imepelekea makampuni mengi kung'ang'ania kwenye blog yake kwa ajili ya matangazo.

Pia amewainspire mablogger wengine ambao wana chipuka kwa kasi ya hatarii kama role models models wao.

Tunamtakia heri na azidi kuendelea kuwa na mafanikio zaidi.
3.5m usd hata kusaga boss wake hana robo ya hiyo pesa,au unaongelea zim $
 
5M USD ni zaidi ya 10B za Kitanzania! Anashindwa nini kuanzisha Radio Station yake?? Ili awe free zaidi na kufanya kazi zake yeye mwenyewe?? Kipindi kama amplifier anachofanya pale Cloud's akihamishie kwenye Radio yake na apige pesa nyingi zaidi??
Ninaona hoja yako, na ina mantiki. Lakini, mambo haya ni complex kidogo. Inabidi mwenyewe atuambie, tena aseme ukweli, kulikoni? Unamfahamu Richard Quest, msoma taarifa za biashara na uchumi pale CNN? Jamaa ni bilionea,lakini ni mwajiriwa wa CNN (Sina hakika kama bado yupo CNN though).
 
Ni mtu wa totoz pia sijui siku hizi. Mwaka 2012 kama sikosei alikuwa anaishi msewe.
Mimi bila kujua tukawa tunafukuzia demu mmoja anaitwa Besta (siandiki zaidi zaidi kuhusu huyu na kilichotokea)
Sasa kumbe demu mmoja tu ndio unasema yeye mtu wa totoz. Hata angekuwa nao watatu sio jambo la kushtusha
 
Naamini Ayo anapesa japo inaweza isifike kiasi hicho...sababu ni kuwa kwa sasa dunia ipo digital zaidi...ndio maana unashangaa kwamba uber hana gari ila anathamani kuliko toyota mwenye magari au facebook ana unautajiri kuliko CNN mwenye masatelite huko anga za juu...so hata Millard ana pesa sababu faida ya digital ni kuwa huna gharama za mitambo za uendeshaji kama traditional radio...

Wasafi wameonyesha hili kwa radio nyingine ndio maana kila radio saa hivi inakimbilia digital platform...

Kingine jamaa ana waandishi kila mahali kuliko clouds...yeye ana break news zaidi ya ITV na waandishi wake...hii inaonyesha amejipanga na ana pesa ya kuwalipa...yote kwa yote dunia kwa sasa ipo digital haitaji kuanzisha radio tena ya fm...kila kitu ni mtandaoni tu.

Big up Millard yuko humble sana.
 
One of the richest bloggers in Africa Forbes ilinukuu.

Ukimuona simple tu wa kawaida lakini ana hela ndeefuuu na nyingi sana.

Utajiri wake unakadiriwa 3-5 Millions US dollars. Vyanzo vingine vya uhakika na kuaminika vinadai anaweza kuwa na utajiri hata zaidi ya iyo dollar million 5.

Ni kwa kujituma kwa Millard na weledi alionao umemfikisha hapa alipo. Ana mchango mkubwa kwenye taifa kwa kutoa ajira hasa kwa vijana na kulipa kodi.

Ubunifu wake na kujituma kwake imepelekea makampuni mengi kung'ang'ania kwenye blog yake kwa ajili ya matangazo.

Pia amewainspire mablogger wengine ambao wana chipuka kwa kasi ya hatarii kama role models models wao.

Tunamtakia heri na azidi kuendelea kuwa na mafanikio zaidi.
Ukiacha bahati na majaliwa Yasir God... Milladi ayo ananidhamu na heshima Sana ..kwenye kazi, kwenye maisha ya kawaida hii ndio Siri ya mafanikio yake..
 
Back
Top Bottom