Millard Ayo, mtangazaji tajiri zaidi Tanzania, analipwa Mil 50-80/month na Youtube

Millard Ayo, mtangazaji tajiri zaidi Tanzania, analipwa Mil 50-80/month na Youtube

Mimi sijapotosha mtu
Nimeongea kile ambacho kinafanyika
Youtube wanalipa endapo tangazo kwenye video yako litaangaliwa angalau kwa sekunde 30 tena utalipwa kwa views 1000 dollar 7 na point kadhaa hivi
Kwenye hayo malipo youtube anachukua 45pc ya malipo yako
Hivyo kwa millardi na diamond kutengeneza hizo hela ni uongo maana sidhani kama wana views za kutosha kiasi hicho
Na wao video zao nyingi hazina matangazo

Kama ingeangaliwa views tu
Justin Bieber angeongoza maana video zake nyingi zinasoma 1bil na kuendelea
Umetudanganya mkuu, fuatilia vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Millard Ayo anamiliki Vifaa vya Redio na Tv kabisa. Akiamua kuweka Transmitter tu anaruka hewani.

Sema kuna kitu anasubiri kitimie.
atasikiliza nani iyo redio.... kumiliki redio sio kama kumiliki iphone 7

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
You tube hutoa royalties ikiwa account yako ina matangazo.Na utapata royalt ikiwa angalau kila tangazo litaangaliwa kwa angalau sekunde 30

Sent using Jamii Forums mobile app
nikionaga ile ads ya tangazo nairusha fasta niende kwenye content ya nilichokusudia kufungua youtube

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
Yaani habari unatoa wewe mwenyewe na kuthibitisha wewe mwenyewe, Milard mwenyewe ndiye alipaswa kusemea hili....hakika umetuona sie Madunya kweli kweli.

You tube haitoi pesa kirahisi hivyo ndugu usipotoshe uma, tena ukizingatia maudhui yaliyopo kwenye channel ni ya nyumbani (local content)...hivyo na Wafuatiliaji kwa 99% lazima watakuwa ni Wabongo..sasa ujiulize ni Wabongo wangapi watatumia muda na MB zao kuangalia tangazo mpaka mwisho...ili hali kuna option ya ku skip au kuondoa?

Pia kumbuka matangazo mengine ni ya kujirudia, sasa ni nani atasubiri aangalie dakika nzima ya kitu ambacho amekwisha kiona hapo kwenye You tube au kwenye TV.

Pesa rahisi anayopata ni kwa yale matangazo anayoambatisha moja kwa moja na video husika, coz mlipaji ni huyo mwenye tangazo na hapo google hawahusiki tena..mfano yale ya GSM.

Namkubali Milard na ningeunga mkono apate kadri inavyowezekana ila sio kuja na habari za kusadikika.

Ingawa kwa kuwa na Watazamaji wengi kunaongeza nafasi ya kupata...kwa mfano kama unaambulia dola moja kwa kila views 5000, ni wazi kuwa ukiwa na views milioni 1 si sawa na mwenye views elfu 50,000....na hapo ukumbuke unapata tu kwa zile video ulizo na haki miliki nazo...sio ilimradi ume upload video basi utavuna pesa.
ndio zangu kuskip tangazo

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
Jamaa anapesa lakini hanenepi unakuta jitu linalipwa laki mbili halafu lina tumbo kubwa alafu linasema hapa kazi tu.

Sent from my Blackberry DTEK70 using JamiiForums mobile app
 
mwenyew nimeshangaa eti analipwa milion tano mawingu hawahawa au

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
Clouds nadhani zaidi ya mshahara ni umaarufu/promotion maana jina lake analotumia clouds ndio jina lake la biashara...kama sio clouds hata blog yake tusingeifahamu kiasi hiki.
 
Clouds kunampa promotion pia, nadhani bila clouds hata hiyo blog yake isingefahamika kama inavyofahahamika, halafu kazi ya utangazaji ni kama part time, maana anaifanya kwa masaa machache sana kwa siku
Mkuu kutangaza ni sehemu ndogo tu ya kazi, sehemu kubwa ni kutayarisha kipindi. Kwa mtu anayeingiza hela hiyo iliyotajwa kamwe hawezi kuhangaika kutengeneza kipindi cha mtu mwingine ili apate mshahara (na promo kama ulivyosema). Hiyo promo kwanza alishapata, haihitaji kwa sasa. Ndio maana wengi wanapinga kwamba anapata kiasi hicho cha hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kutangaza ni sehemu ndogo tu ya kazi, sehemu kubwa ni kutayarisha kipindi. Kwa mtu anayeingiza hela hiyo iliyotajwa kamwe hawezi kuhangaika kutengeneza kipindi cha mtu mwingine ili apate mshahara (na promo kama ulivyosema). Hiyo promo kwanza alishapata, haihitaji kwa sasa. Ndio maana wengi wanapinga kwamba anapata kiasi hicho cha hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
nadhani habari anazotangaza pia zipokwenye blog yake, so kuandaa kuna serve both kazi yakebinafsi na kazi ya clouds, halafu promo hainaga mwisho inahitajika tu, fikiria voda wanafanya promo zote hizo kwenye tv, radio na blogs, mabango, ligi kuu japokuwa wanafahamika na wanaweza kutuma sms pia
 
Back
Top Bottom