Millard Ayo unatuangusha

Kuna kitu kinaitwa conflict of interests kwenye hii mikataba ya ajira. Unapoajiriwa unakubali kabisa kwamba hutafanya biashara au kazi nyingine yenye mlengo sawa na wa ajira yako, hutakiwi kufanya biashara itakayocompete na hiyo ya mwajiri wako.

Habari ya Millard Ayo kuwa na Blog, You Tube na Mitandao mingine ni lazima kwa mujibu wa mkataba asiweke vitu ambavyo vitakinzana na matakwa ya mwajiri.

Kama unaona AyoTV anatumia hadi brand ya Clouds mfano mic nk.
 

Huyu dogo hapo ndipo aliponikera nikaamua kumu unfollow insta
 
Hata mimi nashindwa kushangaa kwa sababu ile millardayo.com ni yake anaingizaje mambo ya kwenye ajira yake na huku kwenye kazi yake ya ziada au mkataba unaingilia hata vitu vilivyo nje ya ofisi zao.

Inawezekana ni ya boss wake ila inatumia jina lake
 
Kwa hiyo mdada kinachomsumbua ni kakiburi ka Kikurya??
 
Wewe sasa ndiye umefafanua kwa mapana yake.
 
Wewe sasa ndiye umefafanua kwa mapana yake.

Unaweza kuona juzi alikuja Neyo akiletwa na Jembe FM, hakuna mahali popote Millard aliandika hii habari, P-Square waliwahi kuletwa na EA Radio, Millard hakuandika hii habari.

Kili Tour huwa inaratibiwa na Kilimanjaro Beer na EA Radio, Millard huwa haandiki chochote kuhusiana na hizo habari. Anaheshimu mkataba.
 
Kama unaona Millard Ayo anakuboa anzisha Channel yako umpost Jide usiwafundishe watu kufanyakazi zao
 
Mkuu huyu anaelewa unachoongea sema anataka akuvuruge na awavuruge watu.

Iyo ni kweli kabisa ishu za Lady Jaydee awajaposti sasa ivi vyombo vya habari vingi vinatakiwa viwe na haki sawa kwa wote.

Tena umenikumbusha Kuna mwimbo uliimbwa na Jaymoo na K-Lyin, tokea K-Lyin aolewe na Mr. Reginald Mengi wa ITV. Nyimbo za Jaymoo sizikiii kabisa zikichezwa na vyombo vya Habari vya itv, EATV na capital TV (IPP media) au ndio kama yaliyomkuta Lady Jaydee
 
Akishatimuliwa ndo ataanza ku-report habari za Jay D si unaona Hando alikuwepo siku yenyewe kwa kifupi adui wa bosi wako ni adui yako ndiyo slogan ya mawingu hata kama hujui hata chanzo cha ugomvi ama huna maslahi na ugomvi wao wewe vunga tu umfurahishe bosi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…