Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo mnamo Januari 21, 2025 amkimshinda
Freeman Mbowe ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kuongoza chama hicho kwa miaka 20.
Mara nyingi kumekuwapo na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikimuhusisha Lissu juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa ndani na nje ya chama chake. Rejea
hapa,
hapa, hapa na
hapa.
Kumekuwapo na
taarifa inayosambazwa mtandaoni ambayo ikidai kuwa Februari 16, 2025 MillardAyo alichapisha taarifa kuwa Tundu Lissu amesema 'No Reforms, No Election' haiwezi kufanikiwa.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa Taarifa hiyo imetengenezwa, Si ya Kweli na haijachapishwa na
Millard Ayo.
Aidha JamiiCheck ilibaini chapisho lililodaiwa kuchapishwa na
Maria Sarungi na kutumiwa katika taarifa hiyo potoshi si la kweli bali lilitengenezwa kwani Maria hakuchapisha kabisa kupitia Mtandao wa X kama inavyoonekana. Hata hivyo kumekuwapo na upotoshaji mwingi unaomhusisha Maria juu ya uwepo wa migogoro ndani ya CHADEMA, rejea
hapa na
hapa.
Hata hivyo akiwa Ikungi mkoani Singida katika
hotuba yake Lissu aliendelea kusisitiza umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kikatiba pamoja na sheria za uchaguzi ili kusaidia uwepo wa uchaguzi mkuu ulio huru na haki huku akipendekeza kusogeza mbele muda wa uchaguzi ili kupisha mabadiliko hayo. tazama hapa kuanzia dakika ya 12:00
View: https://www.youtube.com/live/A9mNhitIz4k?si=t14dTXGZJez1T5HD&t=721