HUYO MTOTO WAKIKE AFANYE BIASHARA INAYOENDANA NA JINSIA YAKE AU MUULIZE ANAPENDELEA KUFANYA KITU GANI?
Hili ndio la msingi,Ila kwanza nimpe hongera sana na mungu akubariki mleta mada kwa kumsaidia dada yako,wengi sana hili hawaliwezi.
Unajua watoto wa kike wengi ni wasiri sana,na kwa age hiyo ya 28yrs ni kwamba lazima atakuwa frustrated na maisha.
Maana mume hana,na maisha yanamzingua,so lazima umsimamie vizuri kwenye maamuzi.
Maana hapo utakuta kwamba ukimuuliza nikufanyie biashara gani,jibu lazima litakuwa,ahhh mie biashara yoyote tu nafanya.Ambapo sio kweli,ni kwamba ukimpa mtaji kwenye biashara asiyo na interest nayo ata atafail tu.
Kwanza tupe record yake kimaisha,na kama ni mdogo wako basi utajua tu kuna vitu gani katika ukuwaji wake alikuwa anavitependa,hobby ya mtu inaanzia utotoni.
Wanawake wengi ni wavumilivu saana wa changamoto za Biashara,ila cha msingi na cha kuzingatia ni kwamba lazima wazo hilo liendane na mazingira,binti wa kike ambae mtaji sio wake,kumpa biashara za kwenda mbali au mazingira hatarishi ni tatizo.Anaweza kufanya biashara za kutoa nje ya mkoa na kurudi,ila kwa malengo kwamba baada ya muda atakuwa sehem moja na biashara iwe tu ni ya kuagiza na kuletewa kisha unaenda tu kwa muda maalum.