Milunda inafaa kuezekea?

Milunda inafaa kuezekea?

wakibisi

Member
Joined
Jan 30, 2021
Posts
18
Reaction score
7
Habari,

Naomba kuuwauliza ndugu zangu, ninategemea kuezeka kakibanda kangu sina pesa ya kutosha kuweza kununua mbao treated hivyo nataka niezekee milunda, naombeni ushauri inafaa kwa ustahimilivu kama wa mbao treated?
 
Inategemea na ukubwa wa nyumba yako na ubora unaoutaka lakini yafaa pia kuezekea
 
Miaka ya nyuma zile kota za NHC Magomeni na kwingineko waliezekea milunda (mikoko), hata nyumba nyingi za zamani Tanga walikuwa waliezekea milunda.
 
Miaka ya nyuma zile kota za NHC Magomeni na kwingineko waliezekea milunda (mikoko), hata nyumba nyingi za zamani Tanga walikuwa waliezekea milunda.
Hiyo ilikuwa zamani, mti unakomaa unakaribia kuwa kama chuma!! Kwa sasa utaipata wapi!! Miti ya aina hiyo??
 
Mkuu inafaa ila hali imekuwa ngumu kiasi hicho mpaka kwenye nyumba yako mweyewe?
 
Bagamoyo hapo nyumba kibao na za kisasa wanaezekea mirunda na fresh tu.
Muhimu nunua ile mirefu wanayotumiaga kuezekea bar za makuti mmoja huwa 5000- 8000.
Hata yangu nina mpango huo.
 
Bagamoyo hapo nyumba kibao na za kisasa wanaezekea mirunda na fresh tu.
Muhimu nunua ile mirefu wanayotumiaga kuezekea bar za makuti mmoja huwa 5000- 8000.
Hata yangu nina mpango huo.
Shukrani sana mkuu nami nipo around maeneo ya Bagamoyo
 
Mirunda labda upate iliyo treated. Ila hii ya mjini hapa ni karagabao baada ya miaka mitatu ndugu mchwa watakutaka uezeke upya....
 
Back
Top Bottom