John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kwa Tanzania kitendo cha kutoa mimba bila sababu za kitabibu ambazo hazikwepeki kufanya hivyo kwa faida ya mwanamke aliyebeba ujauzito ni kosa kisheria.
Pamoja na hivyo, bila kujali mimba imetoka yenyewe au imetoka bahati mbaya au imetolewa makusudi, hiyo haiondoi huduma ambayo mwanamke anatakiwa kuipata kwa faida ya afya yake.
Huduma ambayo mwanamke anatakiwa kuipata kitaalamu inaitwa Comprehensive Post Abortion - (cPAC) ambayo kwa Kiswahili inatambulika kama “Huduma Baada ya Mimba Kuharibika”, hii hutolewa kwa ajili ya kulinda usalama wa afya ya mwathirika wa tukio, wataalamu wa afya wanasema huduma huu ni muhimu sana kwa mwathirika.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama, Elias Kweyamba anataja baadhi ya huduma za cPAC ambazo mwanamke anatakiwa kuzipata ndani ya muda mfupi tangu kuharibika kwa mimba au kutolewa ni:
-Kusafishwa kizazi (usafi wa kizazi), kupewa ushauri wa kisaikolojia, kupewa elimu ya afya ya uzazi
-Kukupewa dawa maalum, kupewa au kuongezewa maji, damu n.k
-Kupewa ushauri wa afya ya kizazi na saikolojia
-Huduma ya kuchunguzwa Saratani ya Shingo ya Kizazi
-Kuchunguzwa Saratani ya Matiti
-Kuchunguzwa magonjwa wa zinaa kama vile H.I.V au gono
-Kuchunguzwa magonjwa ya kuambukiza