Mimba tatu zimeharibika

Kama unaamini katika MUNGU nenda kwa watumishi wa MUNGU wenye nguvu za kiroho wakuasaidie jambo hilo ni dogo sana kwa MUNGU.
 
Njoo kwa Yesu, mtoto atapatikana. Hizo ni laana tu na vifungo vya Ibilisi vilivyomkata huyo mkeo.
 
Aisee ww jamaa unajua sana kumkatisha mtu tamaa asante
 
Aisee ww jamaa unajua sana kumkatisha mtu tamaa asante
Sijakukatisha tamaa bana. Ni kuwa sijaona uhusiano wa mirija kuziba na miscarriage (labda madr watatufafanulia).

Nenda hapo chanika nasikia ni dr mzuri...mwingine yupo arusha. Labda huyo operation itasaidia. Naelewa upo desparate....

Kikubwa nikumtanguliza Mungu.
Pia msiwazie sanaaaa nayo huchangia
 
Kosa kubwa wanalolifanya watu wenye shida ya uzazi ni kuruhusu presha ya mtoto itawale maisha yao, presha ya marafiki, ndugu na majirani haipaswi kuwatawala.

Japo kweli ni stress lakini mnapaswa muweze kuicontain,

Kimsingi hapo pana mambo mawili,
Kwanza inaonekana bibie alikuwa na shida ya mimba kutoka na mimba za chini ya miezi 2 kama nimekuelewa vizuri, hii sio shida sana kwa mimba kutoka miezi mitatu ya kwanza, asilimia kubwa ya kisababishi ni chromosomal abnormalities, mwili unakuwa umeona kuna shida juu ya kiumbe kilichopo na kuamua mimba itoke ili isilete kiumbe cha ajabu, (so mostly is a protective mechanism).

Lakini pia kuna vitu vingine kama maambukizi kama hayo ya Rubella, syphiliis, toxoplasmosis, cytomegalovirus, na Hepatitis.

Pia vitu kama antibodies (antiphospholipids antibodies) huweza kuwa sababu ya mimba hizi kutoka.

Kama alikuwa na Rubella probably ilikuwa inachangia kwenye shida hiyo, ila kwakuwa imetibiwa ni vyema kupima tena na kuhakikisha kuwa hana tena hayo maambukizi,

Chapili inaonekana ana shida nyingine ya mirija ambayo hii husababishwa na maambukizi kwenye njia za uzazi (Pelvic inflammatory disease) hii huweza kupelekea mirija kuziba kabisa na kusababisha asiweze kushika mimba (tofauti na mimba kushika na kutoka).

Kwa maelezo yako inaonekana hapo awali hii haikuwa shida maana aliweza kushika mimba, lakini pia kuziba mrija mmoja bado unabaki mnoja na huo uliobaki unaweza kusafirisha ovum na kutunga mimba.

Swali ni je Maambukizi haya yaliyosababisha mrija kuziba yalitibiwa!??
Kama hayakutibiwa yawezekana yaliendelea na kusababisha mrija wa pili pia kuziba, (NOTE:Maambukizi haya ni tofauti na yale ya Rubella na huwa hayanaga dalili nyingi za kujionyesha au huchelewa kujionyesha)
Na hayo maumivu wakati wa siku zake (dysmenorhoea) moja ya visababishi ni haya maambukizi yani PID,

WHAT TO DO!
Mrudi hospital bila kuchoka maana shida yenu haitibiwi kwa mkupuo, inatibiwa kwa process, inahitajika mfanye Ultrasound tena kuona viashiria vya PID na vikiwepo atibiwe vizuri pia mtapaswa kurudia HSG kuona hali ya mirija, kwakuwa hormone zilikuwa sawa na assuming hamjatumia dawa zozote za ki-hormone hii kwasasa sio ishu,

Baada ya hayo mtapaswa kupata muda wakujaribu kutafuta mtoto haswahaswa kwa kuzingatia zile siku nzuri kwenu kwenye kalenda (ni jambo zuri kuwa siku zake hazibadiliki hovyo)

Majibu ya Vipimo pamoja na matibabu ya vitakavyobainika yatadetermine nini kifuate.

Nakutakia kila laheri
 
Kitu ambacho hujaelewa hata mada yangu nimeongelea kwamba alipata mimba tatu zote zikatoka sasa imekuwa hata kushika mimba hashiki tena baada ya zile kutoka ndio maana nikaweka HSG kipimo kwa hiyo sasa maana yake tatizo limezidi maana mwanzo alishika zikatoka sasa hata kushika hashiki na ndio maana nimesema tumefanya HSG tena mirija yote imeziba kuizibua ushauri niliopewa ni lazima HSG ifanyike au bado na hapo haujaelewa
 
Asante sana kwa ushauri wako wa kitaalamu zaidi kaka Rubella ilionekana tukaitibu tukafanya HSG jibu ni kwamba sasa mirija yote imeziba sasa cha kufanya tuliambiwa lazima ifanyike HSG ila hapo nakushikuru kwa kuniambia nifatilie hiyo PID ambalo hapo kabla sikuwa najua
 
Okay basi ni wazi shida imejulikana,
Ni kweli HSG hutumika pia kama curative japo sio guarantee kuzibua mirija yote, na yawezekana kama nilivyosema alikuwa na PID ambayo haikutibiwa na ikasababisha mrija wa pili nao kuziba so fanya mapema urudi ukafanye hiyo HSG (as a curative procedure) kama itazibuka well n good, atapaswa kutumia dawa pia kuondoa hiyo infection,
Then itabaki kazi yako sasa, 'kulenga'
Pia nakushauri urudi kwa daktari huyohuyo aliyekuambia urudie HSG maana anajua mtiririko mzima ulivyoenda (ni vizuri kama atakuwa ni obstretician/gynaecologist)
 
Asante mkuu ngoja nipambane mpk mwisho ila sitaki kuchepuka mpk nijue hatma ya mke wangu kipenzi ati
 
Ohh haleluyaaa
 
Nimejikuta naimba wimbo huu "Tazama, wewe ni Bwana; Mungu wa wote wenye mwili. Je kuna neno gumu lolote? Usilo liweza? Je kuna neno, kuna neno, kuna neeno? Usiloo liweza? Je kuna neno gumu lolote? Usiloo liweza"
Nilitaka nikupe like hata 1000000000 mpenz, ila nimeshindwa.
 

Braza sijakusoma.muda mkeo sweetlady hajambo hahaha.... kweli muda ndio shida laiti angeweza asisikilize ya watu azidishe upendo kwa mkewe ipo siku Mungu atasikia kilio chake lakini la basi itakuwa kama Mwenyezi alivyopanga
 

Binadamu wachache sana wanaweza kutoa ushauri unaotoka ndani ya moyo wake......nimejisikia hivyo hongera sana kaka umeweza kumpa faraja na kuweza kumsaidia kutokukata tamaa hata kwa kipindi cha miaka ijayo kama atakusoma sawasawa bila shinikizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…