Mimba tatu zimeharibika

Mimba tatu zimeharibika

Ndugu wana JF Doctor nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.

Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.

Nikampelaka Recency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushuka tu imekuwa tatizo.

Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani.

Nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.

Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.
Kama unaamini katika MUNGU nenda kwa watumishi wa MUNGU wenye nguvu za kiroho wakuasaidie jambo hilo ni dogo sana kwa MUNGU.
 
Njoo kwa Yesu, mtoto atapatikana. Hizo ni laana tu na vifungo vya Ibilisi vilivyomkata huyo mkeo.
 
kama operation itasaidia fanyeni. ingawa sioni uhusiano wa mirija kuziba na mimba kutoka. all in all ikishindikana mkafanye IVF, tena kama mna uwezo nendeni nje ya nchi angalau wenzetu hufanya uchunguzi wa kina kabla ya tiba (madr wa bongo msinipopoe mawe ndio ukweli wenyewe) yaani i wish mchunguzwe vizuri wewe na mkeo.
Aisee ww jamaa unajua sana kumkatisha mtu tamaa asante
 
Aisee ww jamaa unajua sana kumkatisha mtu tamaa asante
Sijakukatisha tamaa bana. Ni kuwa sijaona uhusiano wa mirija kuziba na miscarriage (labda madr watatufafanulia).

Nenda hapo chanika nasikia ni dr mzuri...mwingine yupo arusha. Labda huyo operation itasaidia. Naelewa upo desparate....

Kikubwa nikumtanguliza Mungu.
Pia msiwazie sanaaaa nayo huchangia
 
Kosa kubwa wanalolifanya watu wenye shida ya uzazi ni kuruhusu presha ya mtoto itawale maisha yao, presha ya marafiki, ndugu na majirani haipaswi kuwatawala.

Japo kweli ni stress lakini mnapaswa muweze kuicontain,

Kimsingi hapo pana mambo mawili,
Kwanza inaonekana bibie alikuwa na shida ya mimba kutoka na mimba za chini ya miezi 2 kama nimekuelewa vizuri, hii sio shida sana kwa mimba kutoka miezi mitatu ya kwanza, asilimia kubwa ya kisababishi ni chromosomal abnormalities, mwili unakuwa umeona kuna shida juu ya kiumbe kilichopo na kuamua mimba itoke ili isilete kiumbe cha ajabu, (so mostly is a protective mechanism).

Lakini pia kuna vitu vingine kama maambukizi kama hayo ya Rubella, syphiliis, toxoplasmosis, cytomegalovirus, na Hepatitis.

Pia vitu kama antibodies (antiphospholipids antibodies) huweza kuwa sababu ya mimba hizi kutoka.

Kama alikuwa na Rubella probably ilikuwa inachangia kwenye shida hiyo, ila kwakuwa imetibiwa ni vyema kupima tena na kuhakikisha kuwa hana tena hayo maambukizi,

Chapili inaonekana ana shida nyingine ya mirija ambayo hii husababishwa na maambukizi kwenye njia za uzazi (Pelvic inflammatory disease) hii huweza kupelekea mirija kuziba kabisa na kusababisha asiweze kushika mimba (tofauti na mimba kushika na kutoka).

Kwa maelezo yako inaonekana hapo awali hii haikuwa shida maana aliweza kushika mimba, lakini pia kuziba mrija mmoja bado unabaki mnoja na huo uliobaki unaweza kusafirisha ovum na kutunga mimba.

Swali ni je Maambukizi haya yaliyosababisha mrija kuziba yalitibiwa!??
Kama hayakutibiwa yawezekana yaliendelea na kusababisha mrija wa pili pia kuziba, (NOTE:Maambukizi haya ni tofauti na yale ya Rubella na huwa hayanaga dalili nyingi za kujionyesha au huchelewa kujionyesha)
Na hayo maumivu wakati wa siku zake (dysmenorhoea) moja ya visababishi ni haya maambukizi yani PID,

WHAT TO DO!
Mrudi hospital bila kuchoka maana shida yenu haitibiwi kwa mkupuo, inatibiwa kwa process, inahitajika mfanye Ultrasound tena kuona viashiria vya PID na vikiwepo atibiwe vizuri pia mtapaswa kurudia HSG kuona hali ya mirija, kwakuwa hormone zilikuwa sawa na assuming hamjatumia dawa zozote za ki-hormone hii kwasasa sio ishu,

Baada ya hayo mtapaswa kupata muda wakujaribu kutafuta mtoto haswahaswa kwa kuzingatia zile siku nzuri kwenu kwenye kalenda (ni jambo zuri kuwa siku zake hazibadiliki hovyo)

Majibu ya Vipimo pamoja na matibabu ya vitakavyobainika yatadetermine nini kifuate.

Nakutakia kila laheri
 
Sijakukatisha tamaa bana. Ni kuwa sijaona uhusiano wa mirija kuziba na miscarriage (labda madr watatufafanulia).

Nenda hapo chanika nasikia ni dr mzuri...mwingine yupo arusha. Labda huyo operation itasaidia. Naelewa upo desparate....

Kikubwa nikuntanguliza Mungu.
Pia msiwazie sanaaaa nayo huchangia
Kitu ambacho hujaelewa hata mada yangu nimeongelea kwamba alipata mimba tatu zote zikatoka sasa imekuwa hata kushika mimba hashiki tena baada ya zile kutoka ndio maana nikaweka HSG kipimo kwa hiyo sasa maana yake tatizo limezidi maana mwanzo alishika zikatoka sasa hata kushika hashiki na ndio maana nimesema tumefanya HSG tena mirija yote imeziba kuizibua ushauri niliopewa ni lazima HSG ifanyike au bado na hapo haujaelewa
 
Kosa kubwa wanalolifanya watu wenye shida ya uzazi ni kuruhusu presha ya mtoto itawale maisha yao, presha ya marafiki, ndugu na majirani haipaswi kuwatawala,
Japo kweli ni stress lakini mnapaswa muweze kuicontain,

Kimsingi hapo pana mambo mawili,
Kwanza inaonekana bibie alikuwa na shida ya mimba kutoka na mimba za chini ya miezi 2 kama nimekuelewa vizuri, hii sio shida sana kwa mimba kutoka miezi mitatu ya kwanza, asilimia kubwa ya kisababishi ni chromosomal abnormalities, mwili unakuwa umeona kuna shida juu ya kiumbe kilichopo na kuamua mimba itoke ili isilete kiumbe cha ajabu, (so mostly is a protective mechanism)
Lakini pia kuna vitu vingine kama maambukizi kama hayo ya Rubella, syphiliis, toxoplasmosis, cytomegalovirus, na Hepatitis
Pia vitu kama antibodies (antiphospholipids antibodies) huweza kuwa sababu ya mimba hizi kutoka.

Kama alikuwa na Rubella probably ilikuwa inachangia kwenye shida hiyo, ila kwakuwa imetibiwa ni vyema kupima tena na kuhakikisha kuwa hana tena hayo maambukizi,

Chapili inaonekana ana shida nyingine ya mirija ambayo hii husababishwa na maambukizi kwenye njia za uzazi (Pelvic inflammatory disease) hii huweza kupelekea mirija kuziba kabisa na kusababisha asiweze kushika mimba (tofauti na mimba kushika na kutoka)
Kwa maelezo yako inaonekana hapo awali hii haikuwa shida maana aliweza kushika mimba, lakini pia kuziba mrija mmoja bado unabaki mnoja na huo uliobaki unaweza kusafirisha ovum na kutunga mimba,
Swali ni je Maambukizi haya yaliyosababisha mrija kuziba yalitibiwa!??
Kama hayakutibiwa yawezekana yaliendelea na kusababisha mrija wa pili pia kuziba, (NOTE:Maambukizi haya ni tofauti na yale ya Rubella na huwa hayanaga dalili nyingi za kujionyesha au huchelewa kujionyesha)
Na hayo maumivu wakati wa siku zake (dysmenorhoea) moja ya visababishi ni haya maambukizi yani PID,

WHAT TO DO!???
Mrudi hospital bila kuchoka maana shida yenu haitibiwi kwa mkupuo, inatibiwa kwa process, inahitajika mfanye Ultrasound tena kuona viashiria vya PID na vikiwepo atibiwe vizuri pia mtapaswa kurudia HSG kuona hali ya mirija, kwakuwa hormone zilikuwa sawa na assuming hamjatumia dawa zozote za ki-hormone hii kwasasa sio ishu,
Baada ya hayo mtapaswa kupata muda wakujaribu kutafuta mtoto haswahaswa kwa kuzingatia zile siku nzuri kwenu kwenye kalenda (ni jambo zuri kuwa siku zake hazibadiliki hovyo)
Majibu ya Vipimo pamoja na matibabu ya vitakavyobainika yatadetermine nini kifuate,
Nakutakia kila laheri
Asante sana kwa ushauri wako wa kitaalamu zaidi kaka Rubella ilionekana tukaitibu tukafanya HSG jibu ni kwamba sasa mirija yote imeziba sasa cha kufanya tuliambiwa lazima ifanyike HSG ila hapo nakushikuru kwa kuniambia nifatilie hiyo PID ambalo hapo kabla sikuwa najua
 
Okay basi ni wazi shida imejulikana,
Ni kweli HSG hutumika pia kama curative japo sio guarantee kuzibua mirija yote, na yawezekana kama nilivyosema alikuwa na PID ambayo haikutibiwa na ikasababisha mrija wa pili nao kuziba so fanya mapema urudi ukafanye hiyo HSG (as a curative procedure) kama itazibuka well n good, atapaswa kutumia dawa pia kuondoa hiyo infection,
Then itabaki kazi yako sasa, 'kulenga'
Pia nakushauri urudi kwa daktari huyohuyo aliyekuambia urudie HSG maana anajua mtiririko mzima ulivyoenda (ni vizuri kama atakuwa ni obstretician/gynaecologist)
 
Asante mkuu ngoja nipambane mpk mwisho ila sitaki kuchepuka mpk nijue hatma ya mke wangu kipenzi ati
 
Tatizo lako limeshagundulika huna haja ya kuhangaika. Mini Mke Wangu anatatizo kama la Mke wako mrija mmoja umeziba. Alikuwa na tatizo la kuugua kwa masaa yasiyopungua kumi mfululizo anapokuwa mwezini Ila tatizo la maumivu liliisha baada ya kufanyiwa operation ya kuzibua mirija kwa kukata na kuunga tena Ingawa operation hiyo haikufanikiwa. Nyama kubwa ilitolewa wakati wa operation ndio iliyokuwa ikimuumiza. Suala la kushika mimba mwanamke akiwa na mrija mmoja inawezekana Ila ni mtihani sana. Suluhisho la tatizo lako ni kufanya invetro fertilization hii ni kutunga mimba nje na kupandikiza ndani ya mfuko wa uzazi. Mimi Nimepata mtoto baada ya miaka kumi na tano ya ndoa kwa njia nilivyokuambia. Njia hii ni Gharama na Mimi nilifanyia nje ya nchi. Ila kwa uwezo wa Mungu Mke Wangu Alipata ujauzito kwa njia ya kawaida na kupata mtoto baada ya miaka 18 ya ndoa. Kwahiyo usihangaike hiyo ndio hali halisi ni mtihani unaohitaji subira ya Mungu kama huna uwezo wa kufanya IVF kama nilivyofanya Mimi. Ila siku hizi unaweza jaribu hata hapo Kenya kwa Gharama nafuu kati ya Dola elfu sita hadi nane Ila hii nayo ni kujaribu tu unaweza pata au kukosa Mimi nilijaribu mara tano mfululuzo hadi kuja kufanikiwa. Mungu yupo na anatenda mtegemee Yeye.
Ohh haleluyaaa
 
Nimejikuta naimba wimbo huu "Tazama, wewe ni Bwana; Mungu wa wote wenye mwili. Je kuna neno gumu lolote? Usilo liweza? Je kuna neno, kuna neno, kuna neeno? Usiloo liweza? Je kuna neno gumu lolote? Usiloo liweza"
Nilitaka nikupe like hata 1000000000 mpenz, ila nimeshindwa.
 
Miaka minne sio mingi hadi ukate tamaa, kinacho kucost hadi sasa ni pressure uliyonao inayotoka kwa marafiki, ndugu pamoja na majirani wanaokuzunguka. Tuliza akili yako mkuu weka imani yako kwa Mwenyezi Mungu halafu anza kutafuta solution ukiwa na amani moyoni mwako, usipanic hilo ni jaribu lako nawe huna budi kulishinda

Braza sijakusoma.muda mkeo sweetlady hajambo hahaha.... kweli muda ndio shida laiti angeweza asisikilize ya watu azidishe upendo kwa mkewe ipo siku Mungu atasikia kilio chake lakini la basi itakuwa kama Mwenyezi alivyopanga
 
Mimi sio daktari lakini kuziba kwa mirija hakuathiri mzunguko wa mwanamke kwakuwa mke wangu hajawahi poteza mzunguko wake hata mara moja. Nadhani hormones imbalance ndizo zinazosababisha mzunguko kubadilika. Pole sana nakutakia kila la kheri na ukitaka kunishirikisha mimi kikwelikweli katika aina yeyote ya msaada niambie kwakuwa nimeuishi uchungu ulionao kwa miaka kumi tano na siku kumi na tano. Allah atakuafu mtegemee yeye. Kila la kheri katika kila la kheri mnalokusudia kilifanya na Allah awafanyie wepesi juu ya hayo mnayokusudia kufanya na amapatie mama huyo ustaamilivu na wepesi juu ya shida zake. Amen.

Binadamu wachache sana wanaweza kutoa ushauri unaotoka ndani ya moyo wake......nimejisikia hivyo hongera sana kaka umeweza kumpa faraja na kuweza kumsaidia kutokukata tamaa hata kwa kipindi cha miaka ijayo kama atakusoma sawasawa bila shinikizo
 
Back
Top Bottom