Mimba ya nne kujifungua kwa njia ya kisu, nini madhara au athari kwa mama?


Mfano ukaambiwa Ina madhara utamshauri aitoe ama? Huo ushauri alitakiwa aombe kabla hajabeba huo ujauzito.

Issue za mimba na kujifungua salama Huwa ni mipango ya Mungu tu mshauri aanze clinic mapema hayo mengine nature will take it's place.
 
ametoka kujifungua mwaka umepita mtoto wa mwisho na uzao wote ni kisu.
Kwanini kisu kwa watoto wote!?
Huyo mkeo ana tatizo gani kiafya linalofanya ajifungue kwa kisu nyakati zote?

Sasa hivi kuna mtindo umejitoleza wa akinamama kutokutaka kujifungua kwa njia ya kawaida.
Hali hiyo inahatarisha sana uhai wa mama haswa pale anapokutana na daktari asiye makini.
Fani ya udakitari siku hizi imevamiwa na wasaka shilingi wasiozingatia miiko ya kazi yenyewe.
Tuweni makini.
 
Mkuu umeuliza swali nzuri sana, iko hivi mimba ya kwanza alikuwa yupo sawa kabisa nakumbuka nilimpeleka kliniki ya kwanza daktari alisema mkeo yupo sawa nyonga zake zimekaa vizuri wakati wa kujifungua haitakuwa shida kabisa, basi maisha yakaendelea mpaka wakati wa kujifungua, nakumbuka uchungu umempata tulikimbia hospitali mapema sana lakini tulipigwa rufaa hospitali kama mbili mara ya mwisho transfa ya muhimbili mkuu tulipewa.
Yani mambo yalikuwa ovyo ovyo sana mpaka nikashindwa kuelewa nini kinaendelea yani nashindwa kuandika mambo mengine ila ni stori ndefu sana kiufupi ndio ivyo.
Ila wadau wamenipa mawazo mbalimbali nitayafanyia kazi pamoja na kuwa karibu na madaktari ili kujua maendeleo ya mama na mtoto.
 

nimekupata nashukuru 🙂
 
Oh God. Je dr kama uzao wa kwanza nilipata placenta abruption iliyopelekea emergeny cs kuna uwezekano wa tatizo hilo kujirudia uzao unaofuata?
 
Oh God. Je dr kama uzao wa kwanza nilipata placenta abruption iliyopelekea emergeny cs kuna uwezekano wa tatizo hilo kujirudia uzao unaofuata?
cha msingi ni kwamba visababish vya abruption ya kwanza vilijulikana na vilifanyiwa kazi
mfano:
-Kifafa cha mimba (Preeclampsia) *edited thanks Hance Mtanashati
-Matumizi ya Tumbaku na Dawa za Kulevya(ambavyo czani kama unatumia)
-Magonjwa ya Moyo au Magonjwa ya Mishipa ya Damu:
-Ukosefu wa Damu (Anemia):
n.b Kwa mwanawake anaeona dalili za placenta abruption, kama vile kuvuja damu ghafla, maumivu ya tumbo, au kusikia uchungu mkali wa tumbo, ni muhimu kutafuta msaada wa matibabu haraka au kua karibu na kitumo cha afya mda unapo karibia incase of any problem anakimbizwa chap
 
Hakuna namna atazaa kwa njia ya kawaida.

Huyo ataendelea kuzaa tu kwa kisu .
 
sam

samahani na mi naomba kuuliza. je kama nilijifungua uzao wa kwanza op kwa ajili ya complication flani je ni lazima uzao unofuata nimpate Dr yule yule anihudumie.
Sio lazima.

Daktari yeyote utakayekutana naye lazima aulizie mimba iliyopita/zilikuwaje(Past obstretic history) na ulipata changamoto ,ipi zipi kipindi cha ujauzito mpaka ulipojifungua .
 
Huu mwandiko wa Chat Gpt 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Huyu na mumewe washauriwe, waache ujinga, huyu mwanamke anaweza kuja kupoteza maisha.

Waache kuzaa!
 
Umeandika nini hapa?

Pre eclampsia sio shinikizo la juu la damu, shinikizo la juu la damu ni high blood pressure, pre eclampsia ni kuonekana kwa protein kwenye mkojo ambayo mbeleni inaweza ikapelekea akapata kifafa cha mimba (Eclampsia) pale mama mjamzito anapoanza ku fit (convulse).
 
Mungu mmoja atajifungua Salama na hatopata madhara kikubwa aamini kua Mungu anaweza yote asali kwa Imani yake na atashinda na kujifungua Salama bila shida
Acha kushauri upumbavu, mara zote hizo alizoshindwa kujifungua salama huyo mungu mmoja hakuwepo walikuwa ni mungu wawili au?
 
Indication moja wapo ya kufanya CS ni mama kujifungua kwa njia ya CS ujauzito uliopita (Previous CS) kinyume na hapo wamfanyie trial ,haswa kwa hospitali kubwa.
 
Labda mtoto alikaa vibaya (breech), au placenta ilijiachia kabla ya wakati (Abruptio placenta) au kulikuwa na low lying ya placenta karibu na cervix (Placenta previa),maana ki kawaida placenta inabidi ijishikize kwenye fundus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…