Mimba ya nne kujifungua kwa njia ya kisu, nini madhara au athari kwa mama?

Mimba ya nne kujifungua kwa njia ya kisu, nini madhara au athari kwa mama?

Kwanini kisu kwa watoto wote!?
Huyo mkeo ana tatizo gani kiafya linalofanya ajifungue kwa kisu nyakati zote?

Sasa hivi kuna mtindo umejitoleza wa akinamama kutokutaka kujifungua kwa njia ya kawaida.
Hali hiyo inahatarisha sana uhai wa mama haswa pale anapokutana na daktari asiye makini.
Fani ya udakitari siku hizi imevamiwa na wasaka shilingi wasiozingatia miiko ya kazi yenyewe.
Tuweni makini.
Mkuu, nadhan ni kuwakosea watu wa taaluma hiyo! Hakuna chuo kinachomfundisha hvyo Daktari. Tutofautishe tabia ya mtu mmoja mmoja na fani yake
By the way, kama mama atajifungua kwa upasuaji, basi mimba zote zinazofuatia atajifungua kwa upasuaji. Kuna kitu inakutwa, trial of labor after cesarean section/vaginal delivery after cesarean section, ikiwa na maana kwamba mama ajaribu kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji lakini imeonekana kwa wamama wengi, uterus huachia ule mshono wa kwanza na hivyo kuhatarisha maisha ya mama na mtoto . Na hvyo, njia Bora huwa ni kujifungua kwa upasuaji tu hata watoto wanaofuata
Ni vizuri ukawa unapata ushauri au majibu ya kitaalamu kuliko kukaa kusikiliza habari za kwenye vijiwe vya kahawa
 
Mkuu utakuja kumuua shemejj, kama huwezi kumwagia nje, ungevaa ndomu, huwezi basi ungejitahidi upige mzigo siku ambazo si za hatari.
 
Wakuu habari za jioni, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kuna mama ni mjamzito kwa sasa ana watoto watatu lakini ametoka kujifungua mwaka umepita mtoto wa mwisho na uzao wote ni kisu. Sasa swali langu uyu mama alitoka kujifungua mwaka jana na sasa ni mwaka tu umepita sasa sijui niseme bahati mbaya amepata mimba nyingine.

Swali langu kwenu vipi kama akihamua kujifungua je kuna madhara ya kiafya atapata ambayo yatagharimu uhai wake? Au atoe tu huu ujauzito?

Naomba ushauri wenu najua hapa kuna madaktari mbalimbali wenge kujua mambo ya afya.

Karibuni kwa mchango.
Mimba ya nne kwa nini kwanza?

Kuna mashindano ya uzazi?
 
Kutoa nadhani ndo
Nilikuwa nawaza atoe mkuu ndio mana nikasema nililete hapa kwa wataalamu ili nipate ushauri juu ya ili suala mana hii wiki sikuwa na amani kabisa yani mawazo mengi sana mkuu acha tu
Hatari zaidi maana ndo unahatarisha kuchanika kwa mfuko wa uzazi kama ukitumia dawa kutoa mimba
 
Kwan huyo mama hajui kama kuna njia za uzazi wa mpango
Alikuwa anatumia njia za uzaz wa mpango siku akiingia bridi/period basi inaweza kwenda mpaka mwezi bado anavuja yani njia zote zilikuwa zinamtesa sana, ikabidi tuanze kutumia kalenda mwisho wa siku ndio ivyo.
 
Mkuu utakuja kumuua shemejj, kama huwezi kumwagia nje, ungevaa ndomu, huwezi basi ungejitahidi upige mzigo siku ambazo si za hatari.
😄😄 Yani mkuu huwezi amini nilikuwa nakutana nae siku si za hatari yani nashangaa mtu kashapata kitumbo dah sio powa
 
Back
Top Bottom