Mimba za mashuleni zilivyosumbua wazungu na changamoto za kutafuta tatizo

Mimba za mashuleni zilivyosumbua wazungu na changamoto za kutafuta tatizo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Mimba za vijana mashuleni ni tatizo lililo Unix’s sana vichwa vya policy makers, tafiti nyingi zilifanyika na mapendekezo kutolewa. Kwa wazungu mimba za vijana mashuleni ni mzigo wa ziada kwa taifa kwani mtoto na wazazi wake wote inabidi wahudumiwe na serikali kuanzia makazi, chakula, afya na elimu.

Tafiti nyingi zilionyesha wahanga wakubwa wa tatizo hili ni jamii yenye kipato kidogo. Inamaana hili tatizo likiachwa liendelee hii jamii haitakuja kujikomboa kutoka kwenye culture poverty.

Moja ya tafiti ilibaini kuwa mimba nyingi za vijana zilikuwa zinatoka kwenye majengo marefu ya nyumba za council. Wakati wa kipupwe vijana waliochwa nyumbani na wazazi wao kwenda kazini hawa huo na uvivu kutoka nje kwenye baridi kali. Kijana wa ghorofa ya 17 anakwenda kushinda ghorofa ya 3 mchana wote.

Tafiti pia zilibaini kuwa, watoto wanaotoka kwenye familia ambazo mzazi mmoja au wote wawili wana elimu ya chuo kikuu. Watoto hawa mara chache sana kusikia wame acha shule kwa ujauzito. Watoto hawa wakipata mimba huzitoa, hupata msaada wa wazazi kulea mtoto na wakaendelea na shule.

Waliamua kuwa nyumba ndefu zina tenga jamii. Wame acha kuzijenga na zile za zamani nyingi zinavunjwa. Wameamua kuwa na Youth Clubs na Youth Workers katika kila mtaa. Hii ilikuwa mopango ya Labourchini ya Tony Blair. Youth Wokers ni lazima wawe na degree na wawe creative kupanga shughuli za vijana.

Kutoa elimu ya uzazi kwa watoto wa shule ya msingi ilikuwa hatua nyingine. Wazo hili lilipingwa katika shule za dini na hata Baadhi ya wazazi. Lakini katika shule za serikali elimu hutolewa. Mtoto kuanzia miaka 10 anajua mimba ni nini na inapatikana vipi.

Gillick Competence Law inatumika kuwapatia dawa za kuzuia mimba wasichana wa miaka 16 na kuendelea bila wazazi wao kufahamu. Wanaweza kuchomwa sindano kila baada ya miezi mitatu. Au referral kwenye abortion clinic bila mzazi kufahamishwa.

Wanaoamua kuzaa baada ya kupata mimba hupewa msaada wote kipindi cha ujauzito. Wakijifungua ni hiari yao kama watapenda kuendelea na shule aliyopo au anataka kuhama shule.

Gypsy community wamekuwa wanufaikaji wazuri wa mimba za mashuleni. Wao huwaoza mabinti mapema wakiwa bikra. Hivyo binti wa miaka 16 ana mume na akipata mimba anaendelea na shule.
 
Hili suala kidogo ni complicated sana maan kimtazamo wangu naona
60% huchangiwa na mazingira na maisha ya bint anayokulia kma kwao n maskin uwezekan huongezeka

4o% huchangiwa na utashi wa muhusika mwenyew kujua ni nini anataka na hpa ndo kweny mziki haswa maana hpa ndo huamua maisha yote ya muhusika mwenyew

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kubwa kwetu watu weusi ni UNAFIKI.

Chanzo kikubwa cha kumaliza tatizo lolote kwanza ni KUKUBALIANA/KUJUA TATIZO.

Pili, Ni Kukubali Kama Tatizo Limekushinda ili upate msaada.

Hayo yote kwetu yamekuwa ngumu kuyafanya na bahati mbaya hatujui tunataka nini.

Nchi yenyewe haina KANUNI wala UTARATIBU tunafuata tu ATAKAVYOONA NA KUJISIKIA MTAWALA.
 
Trickyy
Japo mazingira yanachangia sana mimba za utotoni

mf familia duni bila shaka wanaongoza
Watt wakike wanaosoma shule za day wanaathirika zaidi kuliko wale wa shule za bweni nk

elimu na kuwalinda watoto itasaidia
Walau binti afike miaka japo 18 tu
 
Hili suala kidogo ni complicated sana maan kimtazamo wangu naona
60% huchangiwa na mazingira na maisha ya bint anayokulia kma kwao n maskin uwezekan huongezeka

4o% huchangiwa na utashi wa muhusika mwenyew kujua ni nini anataka na hpa ndo kweny mziki haswa maana hpa ndo huamua maisha yote ya muhusika mwenyew

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa hata tafiti zinaonyesha neighbourhood inachangia. Binti wa Masaki kupata ujauzito na kuacha shule ni mara cha he sana. Huku kwetu Kwamtogole ni kawaida tu.
 
Hii ngoma nyepesi sana kuicheza ukiwa nje ya dimba ila ingia Dimbani uone Sindimba ilivyo.
 
Back
Top Bottom