Mimi kama muislamu najiuliza, Haji Manara alienda Macca au Makambako?

Mimi kama muislamu najiuliza, Haji Manara alienda Macca au Makambako?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Kwenda macca kwa jambo la kiimani ni ishara kubwa sana kwa muislamu yoyote yule, na lazima tabia zake pia ziakisi heshma ya Macca na uislamu.

Haji Manara alikuwa mwalimu wa madrasa, na amepiga sana madufu na ngoma za daku usiku kucha.

Lakini tangu atoke Macca amekuwa mtu wa hovyo sana, na tabia zake ni matusi kwa uislamu. Anashikana na wanawake hovyohovyo mabarabarani wakiwa uchi wa mnyama, anakutwa na picha za video akiwa na machangudoa naambo mengi machafumachafu.

Alienda Macca au Makambako?
Screenshot_20231224-131352.jpg
1703412782105.png
 
Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa katika Uislam kila amali (tendo) ya mja hulipwa na Mungu kutokana na Nia. Ikiwa alikwenda Makka kufanya ibada ya umrah kwa ajili ya Mungu basi atalipwa kwa nia yake na ikiwa alikwenda kwa ajili ya kuonekana na watu basi vilevile atalipwa kwa nia yake.
Tusisahau kuwa Nia ya mtu ipo moyoni na hakuna ajuaye nia ya mtu isipokuwa Mungu peke yake.

Katika uislam kuna kitu kinaitwa MIZANI. Kwa maana siku ya kufufuliwa watu,Mungu ataweka mizani kwa ajili ya kupima matendo ya waja wake. Kwa maana kila mja ana matendo mema na matendo maovu.

Hivyo wataofaulu ni wale ambao mzani wao upande wa matendo mema utakuwa mzito kuliko matendo maovu na wataopata hasara ni wale ambao matendo yao maovu yatakuwa mengi kuliko mema.

Kwenda kuhiji au kufanya ibada ya Umrah hakumfanyi mwanadamu kuwa MALAIKA! Mlijue hilo.

Unaweza kwenda kuhiji,ukatubu na ukasamehewa dhambi zako zote ila bado ukaendelea kufanya dhambi kwasababu mwanadamu hajakamilika, bado ni mdhambi tu mpaka pale atakapoondoka ulimwenguni. Kinachotakiwa ni kuendelea kumuomba Mungu msamaha na kutubu madhambi yetu kila pale tunapokosea.

Hivyo haji manara hajasalimika kutokana na madhambi licha ya kufanya ibada ya hijjah au umrah,na kufanya madhambi kwake baada ya kurejea katika jiji la makka hakumfanyi kuwa sio Muislam .

NB
Siungi mkono mambo ayafanyao mitandaoni ila nimeelezea jambo hili katika mtazamo wa kiislam
 
Back
Top Bottom