Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa katika Uislam kila amali (tendo) ya mja hulipwa na Mungu kutokana na Nia. Ikiwa alikwenda Makka kufanya ibada ya umrah kwa ajili ya Mungu basi atalipwa kwa nia yake na ikiwa alikwenda kwa ajili ya kuonekana na watu basi vilevile atalipwa kwa nia yake.
Tusisahau kuwa Nia ya mtu ipo moyoni na hakuna ajuaye nia ya mtu isipokuwa Mungu peke yake.
Katika uislam kuna kitu kinaitwa MIZANI. Kwa maana siku ya kufufuliwa watu,Mungu ataweka mizani kwa ajili ya kupima matendo ya waja wake. Kwa maana kila mja ana matendo mema na matendo maovu.
Hivyo wataofaulu ni wale ambao mzani wao upande wa matendo mema utakuwa mzito kuliko matendo maovu na wataopata hasara ni wale ambao matendo yao maovu yatakuwa mengi kuliko mema.
Kwenda kuhiji au kufanya ibada ya Umrah hakumfanyi mwanadamu kuwa MALAIKA! Mlijue hilo.
Unaweza kwenda kuhiji,ukatubu na ukasamehewa dhambi zako zote ila bado ukaendelea kufanya dhambi kwasababu mwanadamu hajakamilika, bado ni mdhambi tu mpaka pale atakapoondoka ulimwenguni. Kinachotakiwa ni kuendelea kumuomba Mungu msamaha na kutubu madhambi yetu kila pale tunapokosea.
Hivyo haji manara hajasalimika kutokana na madhambi licha ya kufanya ibada ya hijjah au umrah,na kufanya madhambi kwake baada ya kurejea katika jiji la makka hakumfanyi kuwa sio Muislam .
NB
Siungi mkono mambo ayafanyao mitandaoni ila nimeelezea jambo hili katika mtazamo wa kiislam