Uchaguzi 2020 Mimi Leslie Oscar Mbena ninayejulikana pia kama Msemakweli Chakubanga, natangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini

You have their vote.
 
Umezaliwa kichangani!! Yaani niliishi hapo miaka mingi ilopita. Diwani akiwa JIKAS aliniuzia sana maziwa kutoka ng'ombe wake bora[emoji23]
 
Wewe unafaa kuwa Rais kweli kweli, cheki na Dovutwa
 
1. Utatumia njia gani kuifanya hiyo morogoro kuwa kama Kariakoo?
2. Je utaweza kupageuza kuwa K/Koo kwa muda gani na kwa bajeti gani?
3. Morogoro mjini kuna changamoto kubwa ya maji, je umeweka mikakati gani kuondoa hilo tatizo?
4. Huduma za elimu na afya ni changamoto haswa magari ya kubeba wagonjwa na vituo vichache vya afya. Umejipanga vp kutatua hilo?
5. Barabara nyingi ni za vumbi una mkakati gani kuboresha?
6. Je una sera gani kuhusu mazingira yaliyoharibika ya Morogoro kama ukipewa dhamana ya kuwa mbunge?
7. Je mipango yako ya kuibadilisha Morogoro inaendana na sera ya uchaguzi ya Chama ya mwaka 2015-20 au umeitoa tu kichwani?
8. Morogoro ni mkoa ambayo ni Big 6 ya kulisha nchi kwa kupitia kilimo. Kwa nini unataka uibadilishe kuwa mji wa wachuuzi tofauti na mipango ya Serikali
9. Je unafahamu kazi za Mbunge ukiwa kama msomi wa Chuo Kikuu?
10. Je mipango unayopanga ina chanzo cha mapato ya kuiwezesha kuifanya na vyanzo hivyo ni vipi?

NAOMBA UYAJIBU HAYO MASWALI KUMI KWANZA
 
Utairudisha Morogoro ile ya awali, hivi mbona husemi Moro ya sasa imehariwa na nani.

Wapiga dili wa CCM wanapotangaza nia ya kugombea ubunge huanza kwa kumsifia JPM then wanajisifia wao 😂

Umefeli bwashee
 
Ila mwenye nchi kasema kuchagua mtu hiyo siku ni kutokana kaamkaje.Swali Je Jiwe anakujua?
 
Morogoro kuna changamoto nyingi zinazokwamisha mzunguko wa pesa na kipato cha mtu mmoja mmoja,ambazo ndizo zinadumaza mji kukua kwa kasi ile ya Mwaka 1970 enzi za akina Mbaraka Mwinshehe.

Changamoto za Morogoro naweza kuziongea toka asubuhi hadi jioni,lakini zipo kero za Msingi kwa sasa, nyingine tayari Serikali ya Ufaransa imeshatoa fungu la Bilioni 175.6 kutoka shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya kutatua changamoto za maji katika Jimbo la Morogoro Mjini na kuwapatia Wananchi maji safi na salama na kuchochea Maendeleo ya kipato cha Mwananchi mmoja mmoja.

Upatikanaji wa maji utaongezeka katika mji wa Morogoro kutoka mita za ujazo 33,000 kwa siku hadi kufikia mita za ujazo 89, 000 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi.

Hiyo ndiyo ilikuwa kero pekee Morogoro Mjini ambayo hadi Mh Kitila Mkumbo ndio kaja kufanikisha hili na Abood yupo,

Zipo changamoto ya barabara za pembezoni kama Lukobe, Mkundi, Tungi, Mzinga na Kauzeni ambazo zinahitaji mtu mwenye maono ya dhati ya Maendeleo kupigia debe bungeni hadi miundo mbinu hiyo ipatiwe fungu la ujenzi.
 
Kuna watu watasema Abood anatoa mabasi ya kuzikia,Abood ametoa ambulance,Abood ana redio na tv lakini hii sio hoja,

Hoja ni kipato cha mtu mmoja mmoja kwa Mwananchi wa Morogoro,ajira hakuna ,hivi ndio vitu vinavyotakiwa vipigiwe kelele ikiwezekana Mh Rais Magufuli achukue Viwanda vyote na vifufuliwe watu wapate ajira. Mh Rais alikuja Morogoro 2016 akasimama Msamvu akasema Viwanda alivyouziwa Abood vianze kufanya kazi mara moja lakini huu Mwaka wa tano Viwanda bado havijaanza kufanya kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…