Uchaguzi 2020 Mimi Leslie Oscar Mbena ninayejulikana pia kama Msemakweli Chakubanga, natangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini

"House Nigger ukimwambia toka ujikomboe atakwambia hapa Mimi nalishwa na mzungu,napewa mkate na maziwa,nikitoka niende kujikomboa nani atanipa mkate na Maziwa!?" - Malcom x
 
Ila kwa taarifa Moro mjini kuna Bwn Abood hapo utafua dafu?

Usije rudi unalialia humu mitandaoni, kila la heri!!
Morogoro Mjini inahitaji mtu mwenye muono tofauti na muono alionao Abood hivi sasa, Abood juzi Kilosa anasimama anasema Mh Rais Wananchi wa Morogoro wamenituma kukushukuru kwa kutuletea ambulance na helikopta kuchukua wagonjwa hospital kubwa kuwapeleka Muhimbili!
 
Haya ukiwa mbunge utasaidiaje upatikanaji wa maji morogoro mjini.
Tayari Bilioni 175.6 zimetolewa kutoka shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya kutatua changamoto za maji katika Jimbo la Morogoro Mjini na kuwapatia Wananchi maji safi na salama na kuchochea Maendeleo ya kipato cha Mwananchi mmoja mmoja,

Upatikanaji wa maji utaongezeka katika mji wa Morogoro kutoka mita za ujazo 33,000 kwa siku hadi kufikia mita za ujazo 89, 000 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi.
 

Sitaki kuwa negative lakini kumuondoa abood morogoro yahitajika nguvu ya ziada maana moro kwa abood sio jimbo pekee. Kiasi flani ni business empire na kaajiri watu wengi tu.

Ukiachana na hiyo misaada, nikiangalia sera yenyewe sidhani kama lay man anaweza kuelewa kama mimi tu na akili zangu za kuvukia barabara nimeshindwa.

Unaenda moro kuwaaminisha watu kuwa wategemee kuwa kkoo ndogo ilhali hao watu kwao dar ni kama Idol. Mtihani huu.

All the best lakini
 
Nakwenda kumhubiria "house Nigger" ajikomboe toka kwa mwarabu,

"House Nigger ukimwambia toka ujikomboe atakwambia hapa Mimi nalishwa na mzungu,napewa mkate na maziwa,nikitoka niende kujikomboa nani atanipa mkate na Maziwa!?"-Malcom x
 

Huyu anatafuta tu uteuzi kwa magufuli kama wale wengine. Kama siyo hivyo, basi atakua hajui namna rushwa sugu ilivyokithiri ndani ya hicho chama.

Ni aghalabu kushinda kura za maoni ndani ya Ccm bila kutoa rushwa, kama baba/mama/ndugu yako siyo kigogo, au kama siyo mtu wa usalama a.k.a uvccm.

Anyway, tunamtakia kila la heri kung'oa huyo Abood hapo Moro.
 
Digrii zote hujagusa UD? Shida inaanzia hapo
Kumbe ili kuwa Mbunge unatakiwa kuwa na digrii ya UD. Sikujua hilo. Mbona Kibajaji wa Mtera ana darasa la saba tu. Mbona Msukuma hana darasa la saba na ni Mbunge. Mbona majimbo kibao tu ni wabunge bila kuwa na digrii na wengi tu wana digrii za vyuo vingine. Hivi na Abood ana digrii ua UD?

Mwacheni kumkatisha jamaa. Aende akajaribu bahati yake.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ mjumbe wa maswali tokea NEC

Everyday is Saturday...........................😎
 
Mkuu ulichosema hapo ni kwamba Mh Rais kafeli, alisema viwanda vifunguliwe na havijafunguliwa, ila wewe ukiwa mbunge viwanda vitafunguliwa.

Boss wako Mkti mtukufu kafeli kumlazimisha mwarabu kufungua viwanda ila wewe utaweza? Unataka kuonyesha una miguvu kuliko yeye?

Aisee, nikushauri ubakie kwanza kuwa mbunge wa Morogoro mjini humu humu JF, ukijifunza kupangua hoja kisiasa miaka mitano ikiisha, ujaribu tena kutangaza nia.πŸ˜€

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Moro iwe k/koo?moro kuna ardhi nzuri ya kilimo, kuna maporomoko ya maji kila kona lakini wananchi wanalia hawana maji safi na salama mimi nadhani ungeanza na mamabo haya kwanza.
 
Hiyo story kwa Morogoro ni mwaka wa 5, hakunagah. Hela ilishatolewa mradi haujawahi kufanywa!

Wewe mjumbe wa CCM Kimara.
Kwa wakazi wa Morogoro watakuambia.
Propaganda za maji, na miradi ya maji, watu wanakula mihela kila siku, maji hayapatikani..Wajanja wamejipatia vibali vya bonde wanaunda vikundi wanachukua maji yao mlimani..

Una taarifa mbunge mtarajiwa..
Wiki 2 sasa tiyari mjini kuna mgao wa maji umeanza..mvua zimekata hazina hata miezi miwili, na zilinyesha miezi karibia 7.

Everyday is Saturday...........................😎
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€kwa mtazamo wako hilo ni kosa?? Yaani hujui Mkiti wako wa Chama anapenda kushukuriwa na kunyenyekewa??

Yaani huwezi siasa, nenda course ya muda mfupi ya how to please & praise ur chairman..

Wenzako wapo kwa kumsifia Mkiti, wewe hutaki unataka kupambana naye??

Daah kila la heri mkuu, hata kama lengo ni kupata uteuzi, ukikosa kupita kura za maoni, kwa mtazamo wako hutoboi naona unafeli kabla hata hujaanza.

Everyday is Saturday............................😎
 
Swali fikirishi

1. Nani atawekeza kwenye bidhaa wanazo/watakazo nunua Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanaopita Morogoro kwasasa, kwenda Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine. 'You have to sell what you know a customer is going to buy not what you think is going to buy'' Swali fikirishi

2. Utakuzaje biashara kwa sera zisizo tabirika ambazo ndiyo chanzo cha biashara nyingi kufa kwasababu huwezi kuendeleza biashara kwa sera za majukwaani (uncertanity policies)
 
Kwanini usiende wanakokujua ukagombee jimbo la Kimara Baruti?
 
Inatakiwa kubadilisha mitizamo ya watu pia 'mind set' swali fikiri je bila mabasi ya Abood hatuwezi kuzikana? mboa zamani tulikuwa tuna zikana, hata sasa bila hayo mabasi tunazikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…