Sipaji jibu kwa nini viongozi mnakumbatia waganga wa kienyeji kwenye nchi.Ninaomba sana watu Hawa wapigwe marufuku wasiwepo Tena.Kwenye hii Karne ya sayansi na technolojia sidhani tunaohitaji Tena waganga wa kienyeji.Ni kundi la watu ambao ndani yake Kuna utapeli usioweza kuelezeka.ili tuepukane na mambo ya ndugu zetu alibino kuwindwa ni heri mambo ya uganga uganga yafutwe kabisa.kama mtu ana ndoto ya kutibu watu basi aende kusomea udaktari kwenye vyuo vinavyotambulika .Tumeacha mambo yameenda kiholela sana,Leo hii ukipita mijini utakuta watu wanajinasibu wao ni watu wenye uwezo wa kutibu magonjwa kwa mitishamba wanauza dawa bila hata kuwa na uthibitisho ni namna gani hyo mitishamba ingeweza kumsaidia mtu